Na,Jusline Marco;Tanga
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Abdul-razaq Badru amesema mamlaka hiyo itashirikiana na wizara za kisekta katika kuhakikisha kijiji cha Msomera Mkoani Tanga kinaendelea kuwa cha mfano kwa kuwekewa miundombinu yote wezeshi kwa ajili ya wananchi wanaohamia.
Akiwa na mwenyeji wake mkuu wa wilaya ya Handeni Salum Nyamwese,wakati alipotembea kijiji hicho kilichopo wilayani Handeni Mkoani Tanga, Kamishna Badru amejionea uendelezaji wa eneo hilo ambalo linatumika kwa ajili ya kuwamishia wananchi wa tarafa ya Ngorongoro wanaojiandikisha kuhama kwa hiari.
“Mheshimiwa mkuu wa wilaya kuna kazi kubwa ambayo serikali imefanya, tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha kijiji hiki kinakuwa bora ili wananchi waliohamia na wale watakaohamia waweze kuishi hapa kwa furaha,”alisema Kamishna Badru.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Handeni Salum Nyamwese alisema kuwa kazi mbalimbali za uboreshaji wa miundombinu katika kijiji hicho zinaendelea ikiwa ni pamoja na ulinzi wa Nyumba ambazo zimeshakamilishwa kujengwa.
0 Comments