Header Ads Widget

MKE AUA MUME KWA KUMCHOMA KISU KISHA NAE KUTAKA KUJIUA KWA SUMU ...


Mkulima wa kijiji cha Ihefu kaya Mdabulo tarafa ya Ifwagi wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Philimon Lalika (49) ameuawa kwa kuchomwa na kisu na mke wake  Elizabeth Kihombo (46)mkulima na kupelekea utumbo kutoka nje.

kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi alisema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 20 mwaka huu katika kijiji cha Ihefu, Kata ya Mdabulo, Tarafa ya Ifwagi Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa. 

Alisema awali marehemu akiwa amelala na mke wake huyo, kulitokea kutoelewana na kupelekea mtuhumiwa kutenda kosa hilo ambapo baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikunywa sumu aina ya Organfosphet (Dawa ya kuhifadhia Nafaka) kwa lengo la kujiua pia.

Pia  Jeshi la Polisi linamshikilia Mtuhumiwa Elizabeth Kihombo, akiwa amelazwa kituo cha afya cha Mdabulo ambapo imebainika chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI