Header Ads Widget

DK.MPANGO AONGOZA HARAMBEE YA ELIMU BUHIGWE

 


Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango (wa pili kulia) akiwaongoza viongozi na wanachi wa wialaya Buhigwe na mkoa Kigoma katika harambee ya  kuchangia ukarabati wa majengo ya shule ya msingi Muhinda na Nyumba za walimu shule ya sekondari Kilelema wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAKAMU wa Rais Dk.Philip Mpango ameongoza viongozi na wananchi wa wilaya Buhigwe na mkoa Kigoma katika harambee ya papo kwa papo kwa ajili ya kuchangia ukarabati wa madarasa ya shule ya msingi Muhinda na ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Kilelema wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Harambee hiyo imefanyika kwenye hafla ya uzinduzi wa benki ya CRDB tawi la Buhigwe mkoani Kigoma ambapo imefanyika  kufuatia benki ya CRDB kukabidhi kwa serikali ya wilaya ya Buhigwe madarasa mawili mapya yenye viti 80 na meza 80 vyenye thamani ya shilingi milioni 60 vilivyotolewa kwa shule ya Msingi Kibande wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango (kulia)  akikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB Abdulmajid Nsekele (kushoto) kwa mchango wake kuchangia miradi ya elimu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma

Makamu wa Raisi, Dk.Mpango ametangaza  kuwa kiasi cha Milioni 246.6 zimekusanywa katika harambee hiyo ambapo kati ya hizo pesa taslim ni shilingi milioni 4.4 kukiwa pia na ahadi za vifaa mbalimbali vya ujenzi vilivyoahidiwa na wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa tawi hilo la benki ya CRDB tawi la Buhigwe lakini pia zipo ahadi ambazo kiasi cha pesa kutaelezwa baadaye.

Akizungumzia makusanyo hayo Dk.Mpango alisema kuwa alilazimika kuelezea kuhusu shule hizo mbili alisema kuwa shule ya msingi Muhinda ni ya muda mrefu na majengo yake yamechakaa sana akieleza pia mahangaiko wanayopata walimu wa shule ya sekondari kilelema ambao hawana nyumba za walimu. 

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya Buhigwe George Mbilinyi (kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango (wa tatu kulia) kuhusu ujenzi wa madarasa mawili yaliyojengwa shule ya msingi Kibande wilayani Buhigwe, meza 80 na viti 80 vyenye thamani ya shilingi milioni 60  vilvyotolewa na Benki ya CRDB

Katika harambee hiyo Makamu wa Raisi aliongoza kwa kuanza kutoa kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo benki ya CRDB ilimuunga mkono kwa kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 100, uongozi wa benki ya CRDB nchini Burundi umeahidi kutoa milioni 30  huku Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim akiahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10.

Baada ya harambee hiyo Makamu wa Raisi ametoa agizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Buhigwe kufungua akaunti ambayo fedha hizo zitahifadhiwa lakini pia kuhakikisha hazitumiki kwa matumizi mengine yeyote Zaidi ya ujenzi kwenye shule hizo na kuonya kwamba hatakubali kuona hata senti moja imetumika tofauti na malengo hayo yaliyokusudiwa.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI