NA MATUKIO DAIMA MEDIA.
Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo Iringa Mchungaji Peter Msigwa amesema ametoka chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha mapinduzi kwa kuwa CHADEMA alikuwa kama mtoto wa mama wa kambo ni ni mama mzazi .
Kuwa siku alipo rudi CCM Rais Samia Suluhu Hassan ambae ni mwenyekiti wa CCM Taifa ndie aliyeongoza wimbo wa mlete MSigwa na vikao vya juu vya chama vimechuja waliokuwa wametia nia ubunge Iringa mjini wote na kuona Msigwa anatosha kuja kuomba ridhaa ya wajumbe ili kuja kuwa mbunge wa Iringa mjini .
Alihoji kama mheshimiwa Rais Samia mwenyewe aliimba MLete Msigwa sasa wajumbe wanamuachaje kwa mfano .
Msigwa akijibu maswali ya wajumbe kuwa iwapo atakosa ubunge ndani ya CCM atahama tena na kwanini amejiunga na CCM .
Alisema hana mpango wa kuhama CCM kwani wakati akiwa mbunge wa Iringa mjini kupitia CHADEMA wao wenyewe CCM walikuwa wakisema Msingwa ni mbunge mzuri sana ila yupo chama kibaya hivyo amekuja chama kizuri CCM anaomba wampe nafasi ili akiwatumikie bungeni .
Msigwa alisema kuwa akiwa CHADEMA alikuwa akiwasumbua sana CCM hadi wakawa wanamuita majina ya ajabu na wakati mwingine walimuita kinyambe kutokana na kuwasumbua ila leo amekuja kuwa mbunge mzuri ndani ya CCM .
Akijinadi katika kata za jimbo la Iringa Msigwa aliwataka wajumbe kuchagua mwakilishi ambaye atawatoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kiongozi anayehamisha fikira namna ya kufikiri na kufanya mambo yao, kiongozi atakayebeba mzigo wa kuwasemea wanachi wake na kuwaletea maendeleo.
"Na hayo nimeyafanya miaka 10 nilipokuwa mbungeni nilipiga kelele nilipokuwa kwa mama wa kambo kwa ugumu lakini nilisimama kwa nguvu kuwasimamia wananchi"
"Nimekuja mbele zenu tena mimi siendi kujifunza bungeni ninaijua vizuri kazi ninayoiomba mkinipa kura nitakuwa msemaji wenu,wakati nipo kwa mama wa kambo nilikuwa na waambia wananchi nini nakwenda kusema bunge na nikitoka nilikuwa naleta mrejesho na maendeleo yalikuwa yanaenda, na ninyi CCM mlikuwa umasema kaMsigwa kanatufaa sana ila kako chama kibaya"alisema
Aliongeza kuwa kwa sasa amerejea chama tawala hivyo anaomba ushirikiano waache kumpigia kura za siri siri bali za wazi kwa kuwa wapo chama kimoja, na kueleza kuwa anao uwezo wa kuleta kura nyingi za Dkt Samia, Madiwani na Mbunge.
Kwa upande wake Mgombea Islam Huwel alisema kuwa hana mengi ya kuzungumza bali amesemama kuomba ridhaa ya wajumbe na kupigiwa kura zote za ndio.
"Mimi sina maneno mengi ya kusema bali naomba ridhaa yenu na kura zenu zoote za ndio ifikapo Agost 4,2025 "alisema Huwel
Huku mgombea Mwingine ni Nguvu Chengula ambae amekuwa akigalagala na kuomba kibali kwa kulia kwa wajumbe.
Nguvu amewaomba wajumbe hao kumpigia kura za ndio ili apate nafasi ya kukipigania chama na wananchi pale atakapofika bungeni.
"Naomba wajumbe wa Ilala mnikumbatie na kunipa heshima ili na mimi nikipata nafasi nirejeshe heshima katika kata za Mkoa wa Iringa, zipo changamoto nyingi kwenye maeneno mengi"
"Watoto wetu wamesoma lakini hawana ajira, wafanyabiashara hawana mikopo wala mitaji,masuala ya miundo mbinu bado ipo katika ajenda ya maendeleo"
Aliongeza 2025 wafanyabiashara watapata mikopo ya halmashauri,ili kuondokana na mikopo ya kausha damu na vimangala na mikopo yenye riba kubwa wakati fedha ipo halmashauri.
Alisema kuwa anaomba apewe nafasi ya miaka mitano ili wananchi waweze kuona radha mpya ya mbunge ambaye alishaanza kutumika hata kabla hajapewa nafasi.
"Naomba kura zenu zote za ndio itakapofika Agosti 4,mimi katika karatasi ya kupigia kura nipo nafasi ya pili hivyo naomba mnione na kunipigia kura niweze kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi"alisema
Mgombea Moses Ambindwile ambae ni wakili amekuwa akitumia uzoefu wake kusaidia wayonge akiwemo mjane Maria Ngoda aliyekuwa amefungwa jela miaka 22 kwa kukukwa na vipande 12 vya nyama ya Swala kisha kumtetea kupitia chama cha mawakili TLS.
Ambindwile alisema kuwa atakapo kuwa kiongozi kama mbunge ataibua miradi ya maendeleo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi, pia kutakuwa na kifurushi cha wajumbe kwa ajili ya kuinuana kimaisha sambamba na wafanyabiashara wadogo wadogo.
"Nitashirikiana na taasisi za fedha kuanzisha saccos ya jimbo lengo likiwa ni kutoa mikopo isiyona riba kwa makundi maalumu, nitawatafutia netwek wasomi ili waweze kupata kazi, nitawawezesha wafanyabiashara kupata mikopo na kushughulikia migogoro yote ya ardhi katika jimbo la Iringa"
aliongeza kuwa kutakuwa na dawati maalumu la kutoa msaada ya kisheria kwa wote ambao watakuwa hawana uwezo wa kuwalipa mawakili na kuhidi kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda usalama wa Mkoa wa Iringa.
Wakati Jesca Msambatavangu ambae ndio Mbunge anayemaliza muda wake alisema kuwa amejipanga kuhakikisha kwamba maisha ya wana iringa yanaboresheka sio kwa kumpa fedha mtu bali kuboresha miundo mbinu inayoweza kuboresha maisha.
"Tunachangamoto kwenye matibabu makubwa kwenye afya hilo serikali inashughulikia, bima za afya zilikuwa zinasumbua tunashughulikia hilo,na tumependekeza mfuko wetu wa bima uweze kutoshereza ili kuwasaidia wananchi kupata matibabu ya uhakika"alisema
Naye kada wa CCM Fadhili Ngajilo alitumia jukwaa hilo kueleza mambo mazuri atakayofanya ambayo ni pamoja na kuwa daraja kati ya wananchi chama na serikali na vyombo vingine vya maendeleo.
MWISHO.
0 Comments