Na mwandishi wetu
Jeshi la Polisi nchini, limetoa tamko kuelekea uzinduzi wa
kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazotarajiwa kuzinduliwa kuanzia kesho Agosti 28,
2025.
Akizungumza na waadishi wa Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David
Misime amesema kuwa jeshi la polisi lipo
tayari na limejiandaa vizuri ipasavyo kuhakikisha linaendelea kuimarisha
usalama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni.
“Jeshi la polisi Tanzania lingependa kuwafahamisha watu wote
kuwa limejipanga vizuri kuendelea kuhakikisha usalama unaendelea kuwepo kabla
ya kampeni na baada ya kampeni,Jeshi la polisi linatoa wito kwa wagombe na
wadau wake wote kwa ujumla kukumbuka kuwa jukumu la kudumisha Amani,Utulivu na
Usalama ni letu sote kama watanzania na
kamwe asiwepo mmoja wetu akawa chanzo cha kukiuka Sheria, Kanuni na Taratibu wakati
wote wa kampeni na baada ya kampeni ili kuepuka vurugu au uhalifu wa aina
yoyote ile kutokea.
Pia ameongeza kuwa kila mmoja anatakiwa azingatie ratiba na muda wa kampeni aliopangiwa ili kupunguza na kuepuka migongano kipindi
ambacho kampeni hizo zitaanza.
“Pia kila mmoja wetu anatakiwa azingatie ratiba na muda wa
kampeni aliopangiwa na kuweza kufika
katika eneo ambalo amepangiwa ili kuepuka migongano na mitafaruko au uhalifu wowote
kuweza kutokea na sisi kama jeshi la
polisi hatutasita kumchukulia hatua mtu
yoyote atakayeonekana analengo la kuvunja Amani kama seheria za Nchi zinavyoelekeza.
0 Comments