NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Watia nia wanaowania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea udiwani katika kata za jimbo la Ismani mkoani Iringa wametakiwa kuwa watulivu katika kipindi hiki kwa kuwa matokeo hayo ni ya awali na hakuna mshindi hadi pale vikao vya chama vitakaporudisha rasmi jina la mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29 2025.
Ushauri huo umekuwa ukitolewa na wasimamizi wa uchaguzi wa chama hicho na kusema kuwa mchakato ulioisha ulikuwa ni wajumbe kuangali ni mtu gani atakaefaa lakini vikao vitaangalia katika vigezo vyake kuona mgombea aliyekidhi vigezo vya CCM katika kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu.
Kwa kuangazia matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni katika kata mbalimbali leo tutakuwa na matokeo kutoka kata za jimbo la Isimani wilaya ya Iringa vijijini, ambapo katika kata ya Mahuninga aliyeongoza katika kura za maoni ni Michael Vahai aliyepata kura 239 akifuatiwa na Jackson Maitei aliyepata kura 111 nafasi ya tatu ikishikwa na Ezekia Mage kura 89 kata ya Mlowa Ismail Lawa amekuwa kinara kwa kupata kura 396, Charles Nyagawa kura 271, nafasi ya tatu akiwa ni Isaka Madege aliyepata kura 37.
Matokeo mengine ni kata ya Ilolompya ambapo mtia nia Patrick Mhegele ameongoza kwa kupata kura 288 akifuatiwa na Elia Kidavile aliyepata kura 159 nafasi ya tatu ikishikwa na Erick Sailutye aliyepata kura 18 na nafasi ya nne akiwa Nipa Utago aliyepata kura 04 na nafasi ya tano nay a mwisho akiwa Nuhu Nzalamoto aliyeambulia kura moja kutoka kwa wajumbe wakati katika kata ya Mboliboli Yusuph Msamba Msamba akiongoza kwa kupata kura 149, akifuatiwa na Khalfani Lulimi aliyepata kura 110 nafasi ya tatu ikishikwa na Asha Mafunde akipata kura 04 nafasi ya nne ikishikwa na Elia Mpogola alimepata kura 01 na nafasi ya mwisho ikishikwa na Mario Gomangulu ambaye hakupata kura hata moja.
Wakati huohuo kata ya Kising’a imemtangaza Ritta Mlagala kuongoza kwa kupata kura 308 wakati Uwezo Nyalusi akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 171 na Athumani Kaita akishika nafasi ya tatu kwakupata kura 19 wakati kata ya Idodi aliyekuwa diwani wa kata hiyo Julius Mbuta ametetea nafasi yake kwa kuongoza kwa kupata kura 391 Sophia Msekwa akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 250 na Bahati Ngetwa akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 73
Katika kata ya Nyang’oro Eliza Ngole ameongoza kwa kupata kura 304 Daudi Ngoti akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 121 nafasi ya tatu ikiwa ameshika Emmanuel Myoka aliyepata kura 78 wakati nafasi ya tatu ikiwa imeshikwa na Ditrick Mwenda aliyepata kura 49 na nafasi ya tano nay a mwisho ikishikwa na Daud Madugulu aliyepata kura 17.
Na katika kata ya Migoli wagombea walikuwa watano ambapo Fatuma Gedi ameongoza kwa kupata kura 257 nafasi ya pili ikishikwa na Mashoto Kivaye aliyepata kura 151 huku nafasi ya tatu akishika Jermia Mkobo aliyepata kura 125 huku John Nzwaga na Joshua Mbalinga wakifungana kura kwa kupata kura 86 kila mmoja.
Kwa upande wa kata ya Mlenge wagombea walikuwa wanne ambapo Fundi Mihayo ametangazwa kuongoza kwa kupigiwa kura 440 na kufuatiwa na Msafiri Nzalamoto aliyepata kura 346 nafasi ya tatu ikishikwa na Kazaroho Duma aliyepata kura 36 na Adela Chatila akishika nafasi ya nne kwa kupata kura 21 wakati katika kata ya Izazi wagombea ni watatu na Constatino Makala akiongoza kwa kupata kura 155 nafasi ya pili akiwa Medson Pila aliyepata kura 150 na nafasi ya tatu akiwa ameshika Habibu Nziku aliyepata kura 68.
Katika kata ya Malengamakali wagombea walikuwa wawili ambapo Stephano Mkissy akipata kura 514 wakati samweli Mbande akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 99, na kwa kata ya Itunundu watia nia walikuwa wanne huku wajumbe wakimpigia kura 135 na kuongoza Nasibu Ngili nafasi ya pili akiwa ni Jella Lukinga aliyepata kura 135 wakati nafasi ya tatu akiwa Hassan Danda aliyepata kura 71 wakati Monica Kamage akifunga hesabu yakuwa nafasi ya nne kwa kupata kura 06 wakati kata ya Kihorogota Mchael Mgongolwa ameongoza kwa kupata kura 332 Ponsiano Kayage akiwa nafasi ya pili kwa kupata kura 183 na nafasi ya tatu akiwa ni Henry Mjema aliyepata kura 20.
Baada ya kutamatika kwa mchakato huo wa awali wa kura za maoni muhimu itakayofuata ni Kamati za Siasa kuwajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya kata.
0 Comments