Header Ads Widget

CCM,CNDD WAPONGEZA UJENZI SGR UVINZA HADI MUSONGATI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa Kigoma kimesema kuwa uwekaji jiwe la msingi kuanza kwa  ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Msongati mkoa Burungu jamhuri ya Burundi hadi Uvinza mkoani Kigoma Tanzania ni mafanikio makubwa kwa chama hicho katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, jamal Tamim akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwekwa jiwe la msingi la mradi huo katika hafla iliyoongozwa  na Raisi wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na Waziri Mkuuwa Tanzania , Kassim Majaliwa akimwakilisha Raisi Samia Suluhu Hassan wa Tanzania katika eneo la Msongati mkoa wa Burungu nchini Burundi  alisema kuwa utekelezaji wa ilani umefanya kazi kwa vitendo.


Tamim alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kuna manufaa makubwa kiuchumi kwa serikali za nchi hizo mbili lakini Zaidi manufaa hayo yanagusa moja kwa moja uchumi wa wananchi wa nchii hizo katika kufanya shughuli za biashara na uchumi.

Jamal Tamim Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma

Akizungumza katika uwekaji huo wa jiwe la Msingi  Bizimana Filemon kiongozi wa Chama cha CNDD-FDD mkoa Burungu alisema kuwa ujenzi wa mradi huo unaimarisha mahusiano yao kama nchi kwa kupitia serikali zao lakini unaimarisha pia uhusiano wa kisiasa baina ya vyama tawala katika nchi hizo mbili.

Filemon alisema kuwa uwepo wa reli hiyo utarahisisha usafiri wa haraka wa abiria na mizigo kutoka nchini humo kuelekea Tanzania hadi bandari ya Dar es salaam ambayo ndiyo kiungo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi hiyo na kwamba uchumi wa Burundi kwa kupitia mradi huo utakuwa kwa haraka.


Akitoa hutoba kwa niaba ya Raisi Samia wakati wa uzinduzi wa mradi huo Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema kuwa mradi huo utachochea ukuaji wa uchumi kwa nchi hizo mbili, kuchochea ukuaji wa uchumi wa kikanda kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo utakuwa kichocheo kikubwa katika ukuaji wa sekta ya biashara, kilimo, viwanda na  madini.

Akizungumza katika Hafla hiyo Raisi wa serikali ya Burundi, Evariste Ndayishimiye alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo ni jambo kubwa kiuchumi kwa nchi hiyo katika kusafirisha mizioa hasa madini ya Nikel ambayo yanapatikana kwa wingi katika enei hilo la Msongati mkoa Burungu nchini  Burundi lakini hayakuwa yakichangia sana uchumi wa nchi hiyo kwa kukosa miundo mbinu ya kuyasafirishia.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI