![]() |
Butembo |
NA. MWANDISHI WETU.
Hatimae mchakato wa kura za maoni ya uchaguzi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Magomeni Mkoa wa Dar es salaam umefika tamati ambapo katika kugombea nafasi ya Udiwani wa Kata hiyo Noordin Yusuph Hassan 'Butembo' ameibuka kidedea kwa kupata kura 149 na kuwashinda wenzake wawili Athuman Mohammed Sheka 'Muddi Mizungu' na Abdallah Mangala.
Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo, Msimamizi Mkuu wa Kata ya Magomeni, Bi. Stella Nyasulu amesema huo ni mchakato wa ndani wa awali hivyo usiwagawe wananchama huku akiwataka wale ambao kura zao hazijatosha kuendelea kutoa ushirikiano ili chama cha mapinduzi (CCM) kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Akitangaza matokeo hayo, amesema Athuman Mohammed Sheka amepata kura 72, Abdallah Mangala 133 na Noordin Butembo kuibuka na ushindi kwa kura 149
Aidha, upande wa kura za nafasi ya Ubunge kwa Kata hiyo, Jimbo la Kinondoni ambao walikuwa wagombea 8, ambapo
Michael Wambura amepata kura 0, David Kitoto kura 0, Wabota kura 1, Alfan 1, Nyamwija 72, Idd Azzan 77, na Abbas Tarimba kura 192.
Noordin Butembo ni kada wa CCM ambaye awali alikuwa akikitetea kiti hicho cha Udiwani, 2020-2025.
0 Comments