Header Ads Widget

BREAKING:MGOMBEA WA CHAUMA UBUNGE IRINGA MJINI AJIONDOA CHAUMA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA

ALIYETEULIWA na chama cha ukombozi wa umma (CHAUMA) kuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Vitus Nkuna ametangaza kujiondoa kushiriki uchaguzi mkuu  huo kwa namna yoyote ile.

Nkuna kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa kwa heshima ya kipekee kabisa ninawashukuru viongozi wa CHAUMA kwa ujumla .


"Nitaendelea kuwaheshimu kama marafiki na walezi wangu (NAJITOA CHAUMA)kwa sasa naelekeza jitihada zangu zote katika shughuli za kijamii na familia Nitakuwa Active Citizeb aluta Continua"

Hata hivyo Matukio Daima Media ilipomtafuta kwa njia ya simu majira ya saa 6:05 mchana wa leo Jumanne Agosti 26/2025 ili kuhojiana zaidi alisema hana nafasi hiyo kwani anatoka mjini kwenda nyumbani na kuwa taarifa hiyo ni sahihi hana cha kuongeza.

"Sitashiriki uchaguzi kwa namna yoyote ile sio kugombea wala kufanya kampeni elewa hivyo"alisema na kukata simu.







JNDSHOPPING BAG VIFUNGASHIO BORA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI