Na Fatma Ally Matukio na Habari App
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Shirika la Maendeleo ya Petroli na Gesi (TPDC) Maria Mselemu amesema Shirika hilo limeibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za Serikali katika utendaji kazi bora.
Akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo lililopo katika maonyesho ya 49 ya kimata ya biashara amesema kufuatia utendaji kazi wa shirika hilo umewafanya kuibuka kidedea kwenye maonesho hayo.
Amesema kuwa, wamekua wakifanya vizuri kwenye maeneo tofauti tofauti ikiwemo mazingira, nishati safi ya kupikia hivyo kupelekea kuwa tuzo hiyo kuwa ya tano
"Kwetu hii ni tuzo ya tano kwenye maonesho haya lakini sisi kwetu hii ni kawaida kwani tumekuwa tukipata tuzo kwenye maeneo taofauti ikiwemo tuzo ya mazingira "amesema Mselemu.Amesema tuzo hiyo ya mazingira wameipata kufuatia matumizi ya nishati safi ya kupikia wameweza kuondoa hewa ukaa kwa tani laki moja.
"Kwa kutumia nishati safi ambayo tunaweka kwenye magari lakini pia kupikia pia kufanyakazi kwa umakini ndio kichocheo cha kutufanya kuwa kinara na hata kupatata tuzo kadhaa"ameongeza.
0 Comments