Header Ads Widget

MAAJABU YA KIJANA ANAYECHORA RAMANI KWA KUTUMIA MIGUU

Na Fatma Ally Matukio na Habari App

Katika kuhakikisha vijana wanapata ajira Chuo Cha Ufundi stadi (VETA) kimekua kikitoa fursa mbalimbali kwa vijana wa rika tofauti ili waweze kujikomboa kiuchumi na kujipatia kipato.


Ukosefu wa ajira imekua ni changamoto kubwa inayowakabili vijana wengi, Joseph Joachim Mtei anaeleza namna alivyoingia Veta na kupata ujuzi wa kuchora ramani za majengo kwa kutumia miguu .


"Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Cha Ufundi stadi VETA Dodoma, ni mlemavu ambae sina mikono lakini natumia miguu yangu kufanya shughuli zangu za uchoraji wa majengo".amesema


Aidha, ameishauri jamii kuacha kuwaficha watu wenye ulemavu nabadala yake wawapeleke VETA wapate ujuzi utakao wasaidia kujikwamua kiuchumi.


Rai hiyo, ameitoa wakati akizungumza na Mtandao wa Matukio Daima Media alipotembelewa katika banda la Veta lilikopo katika maonyesho ya 49 ya kimataifa ya biashara (Sabasaba).


Aidha amesema amekwenda katika maonesho ya Kimataifa ya kibiashara maarufu kama Sabasaba kuwaonesha watanzania wenzake kuwa wasiwafiche watoto wenye ulemavu,au wale wana viungo vyote lakini wamekata tamaa kwa kuona kwamba hawawezi kufanya chochote wanaweza kujiunga na VETA nakupata ujuzi wa fani mbalimbali. 


"Wakija VETA hawawezi kukosa cha kufanya,watafanya kila kitu kwasabubu kama darasani wameona hakuna Cha kufanya,VETA wanafundisha kwa vitendo kwani hawa angalii uelewa wako wa darasani wana angalia matendo yako ambayo yatakufanya uweze kufanya kile ambacho wewe una uwezo nacho."amesema Joseph


Amesema kuwa, ameenda VETA akiwa hajui kabisa kuchora ramani za Majengo ila kwa vile walimpa mafunzo na ujuzi sasa hivi ana uwezo wa kuchora ramani ambayo anaweza akaiuza kabisa akapata kipato


Hata hivyo Mtei amesema kwamba ramani haiwezi kuchorwa kwa siku moja na kuimaliza,inachukua muda,ili ramani ikamilike unaweza kutumia wiki moja,mbili hadi wiki tatu.


"Naishukuru VETA kwa kunikubalia kujiunga kwa ajili ya kupata ujuzi huu,kwani hawakuona kwamba mimi nilemava ambaye sina mikono labda nitakua mzigo kwa walimu walinichukulia kama wanafunzi wengine"


"Nilianza VETA Mwaka wa kwanza 2024 na sasa nipo Mwaka wa pili,nafurahia sana kwasabubu sasahivi nina uwezo wa  kuchora ramani yoyote pasipo changamoto yoyote,sasahivi siwezi kuwa tegemezi tena kwa jamii au familia yangu,nauwezo wa kukitegemea mwenyewe."ameleza

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI