Header Ads Widget

UMOJA WA MATAIFA WALAANI YA WATU ZAIDI YA 40 DR CONGO


 "Ujumbe walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) Umelaani vikali shambulio lililotokea usiku wa Julai 26 hadi 27, 2025, huko Komanda, takriban kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, mji mkuu wa Ituri", taarifa ya MONUSCO kwa vyombo vya habari imesema.

Taarifa hiyo ya MONUSCO iliongeza kusema kuwa , " Kulingana na ripoti rasmi, shambulio la wanajeshi wa ADF lilisababisha vifo vya raia wasiopungua 43 wakiwemo wanawake 19, wanaume 15, na watoto tisa, huku watu kadhaa wakitekwa nyara.

Nyumba na maduka pia yalichomwa moto, na kuzidisha hali mbaya ya kibinadamu ambayo tayari inaripotiwa katika jimbo hilo"

Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo walisema kwamba raia waliohudhuria ibada ya mkesha katika kanisa la eneo hilo walikatwa kwa mapanga, na kusababisha vifo vya watu hao. Wengine kadhaa walijeruhiwa vibaya.


Luteni Jules Ngongo, Msemaji wa Jeshi la Congo katika jimbo la Ituri, ambako shambulio hilo lilitoke alisema Jumapili kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye X kwamba jeshi la Congo linasema mauaji haya yalitekelezwa na Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye silaha la kigeni linalotoka Uganda linaloendesha harakati zake katika jimbo wa Ituri.

Luteni Ngongo alisisitiza kuwa shambulio mauaji hayo yalikuwa ni lilikuwa kitendo cha kulipiza kisasi kinacholenga kugeuza operesheni ya pamoja ya kijeshi inayoendelea inayowalenga ADF na Vikosi vya DRC na Vikosi vya Ulinzi vya Wananchi wa Uganda (UPDF).

Mnamo tarehe 23 Julai, MONUSCO iliwatuhumu ADF kufanya shambulio lingine lililowauwa raia 47 huko Eringeti, pia katika jimbo la Ituri, kati ya Julai 8 na 9, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI