Header Ads Widget

TMDA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NDANI YA SABASABA


Na Andrew Chale, Matukio Daima App Dar 

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Imeendelea kutoa Elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa na vitenganishi ndani ya maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara (SabaSaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Temeke, Dar Es Salaam.

Akizungumza katika banda la Stone town ndani ya maonesho hayo ya Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amesem kama Mamlaka  mara kwa mara wataendelea kutoa elimu kwa Umma  ili kusaidia Jamii kuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya Dawa,

Amesema majukumu makubwa ya TMDA ni kusajili dawa za ndani na zinazotoka nje kuingia nchini hii ni pamoja na kufanya ukaguzi kila siku ikiwemo kwenye maduka ya Dawa, masoko na mipaka ili kumlinda mtanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo (Kushoto), akitoa elimu na kugawa kipepelushi cha elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa na vitenganishi kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) ndani ya banda la Stone town katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.


"Sisi jukumu letu kuhakikisha kwamba dawa inatumika kama ilivyokusudiwa na sio kumdhuru mtumiaji.

Majukumu yetu ni kuhakikisha tunasajili dawa zilizosajiliwa na kukidhi soko la nchi yote hii ni kumlinda Mtanzania katika usalama wa dawa hivyo tunahakika ubora na ufanisi.

Vile vile tunafanya kazi tunapima bidhaa za dawa kupitia Maabara zetu za kisasa ambazo zina ubora wa Kimataifa wa WHO". Amesema Dkt. Adam Fimbo.

Aidha, katika banda hilo la TMDA, Dkt Adam Fimbo ametoa elimu kwa Wananchi waliotembelea juu ya matumizi sahihi ya Dawa na kuacha kutumia bidhaa hiyo kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu ili kuepuka usugu wa dawa.





Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Umma TMDA) Gaudensia Simwanza (kushoto) akitoa elimu kwa Wananchi ndani ya Banda la Stone town la maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Saba Saba.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI