Everton ina nia ya kumsajili kiungo wa Uingereza Jack Grealish, 29, kwa mkopo lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa West Ham na Napoli. (ipaper - usajili unahitajika)
Alexander Isak, 25, ameidhinisha masharti ya kibinafsi na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano ikiwa ada itakubaliwa kumsaini mshambuliaji huyo wa Newcastle na Uswidi. (Sky Sports Uswisi - kwa Kifaransa)
Brentford haiko tayari kumtoa mshambuliaji wa DR Congo Yoane Wissa, 28, kwa Newcastle kwa bei yoyote isipokuwa wasajili kwanza mbadala wake. (ipaper - usajili unahitajika)
Manchester United imejiunga na mbio za usajili wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 22, ambaye pia yuko kwenye mazungumzo na Newcastle. (Sun)
Chelsea inakaribia kufikia makubaliano ya zaidi ya euro 40m (£34.8m) kumsajili beki wa Uholanzi Jorrel Hato, 19 kutoka Ajax. (Athletic - usajili unahitajika)
Manchester United imewasilisha dau la euro 40m (£35m) kumsajili kiungo wa Sporting Morten Hjulmand, 26, lakini klabu hiyo ya Ureno inataka euro 50m (£43.4) kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark, ambaye pia ananyatiwa na Juventus. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Nottingham Forest inawania kumsajili winga wa Fulham na Uhispania Adama Traore, 29, ambaye aliwahi kucheza chini ya ukufunzi wa kocha Nuno Espirito Santo katika klabu ya Wolves. (Telegraph - usajili unahitajika)
Forest pia iko mbioni kumsaini mchezaji wa kimataifa wa Uswizi Dan Ndoye, 24, kwa kandarasi ya muda mrefu baada ya kufahamisha Bologna kuhusu nia yake ya kujiunga na Ligi ya Premia. (Telegraph - usajili unahitajika)
Ikiwa Forest itaipiku Napoli kupata saini ya Ndoye, klabu hiyo ya Italia huenda ikafufua mpango wa kumsajili Grealish wa Manchester City au mshambuliaji wa Manchester United na Argentina Alejandro Garnacho, 21. (Sun)
Chelsea hawana nia ya kumuuza beki wa Uhispania Marc Cucurella, 27, huku tetesi zikiibuka kuwa anafuatiliwa na vilabu vya Saudi Arabia. (Football London)
Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Morgan Rogers, 23, ananyatiwa na Chelsea na The Blues wako tayari kumpa mlinzi wa Uingereza Tosin Adarabioyo, 27, na mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, ada ya kupata mkataba. (Football Insider)
Bayern Munich ndio klabu pekee iliyoonyesha nia ya kumsajili kiungo wa RB Leipzig Xavi Simons, 22, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anavutiwa zaidi na Ligi ya Premia. (Bild - kwa Kijerumani)
Klabu za Liverpool, Everton, Aston Villa na Bournemouth huenda zikamkosa Mfaransa Nathan Zeze,20, huku mlinzi huyo wa Nantes akipendelea kuhamia Neom SC ya Saudi Pro (Sun)
Everton, West Ham na Nottingham Forest wanapigania kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 27, ambaye anataka kuondoka Juventus msimu huu wa kiangazi. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Kiungo wa Manchester United Muingereza Toby Collyer, 21, yuko tayari kuondoka Old Trafford kwa mkopo baada ya kucheza mechi 13 msimu uliopita. (Daily Mail)
0 Comments