Header Ads Widget

AZAM FC WAMTENGEA MAMILION FEISAL SALUM KUSALIA CHAMAZI


 Na Leonard johnson

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam fc upo Katika Harakati za kuhakikisha wana Mbakisha kiungo wao fundi Feisal salum(27),Katika klabu Hiyo Mara baada ya mkataba wake kumalizika na Hadi hivi sasa akiwa bado haja saini mkataba Mpya .

Taarifa  zinaeleza kuwa uongozi wa Azam fc umempa Fei ofa ya Mkataba mpya ambayo ni "TAKE IT or LEAVE IT ",Ambapo Azam fc wapo tayari kumpa Fei hela binafsi ya kusaini mkataba mpya [sign on fee Tsh 800m cash],mshahara wa (Tsh 50m take home )kwa mwezi na hii ni baada ya makato na kodi.

Hivyo  kiujumla Fei atalipwa kwa mwaka pesa yenye thamani ya Tsh 200m ,hii nikuzuia mianya ya vilabu vingine kuweza kumpata kiurahisi ,kwa kawaida ili klabu nyingine ziweze kumpata Feisal zinatakiwa kuwa na Bilion 2...watoe 1.3b ya Azam kisha Fei wampatie sign on fee yake ya Tsh 800m
Ikumbukwe kwenye mkataba wa Feisal na Azam kuna "Buy out" clause ya dola 500.000[tsh1,285,000,000]kama  fei atahitaji kuvunja mkataba wake ,hapo atakuwa huru kuondoka klabuni hapo .

Hata hivyo kwasasa kiungo huyo anahusishwa moja kwa moja na klabu ya simba sc, kwani ni mmoja wa wachezaji wanao pigiwa chapuo kubwa kujiunga na klabu hiyo ambayo kwa sasa inafanya maboresho yake makubwa kuhakikisha ina rejesha heshima yake katika utawala wa soka la ndani. 

Mpaka hivi sasa hatma ya Feisal salum haijajulikana kama ataondoka Azam Fc au kuendelea kusalia   kikosini hapo kwa sababau bado haja saini mkataba mpya na klabu yoyote .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI