Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB),imemshukuru Rais Samia Sulunu Hassan kwa kuipa fedha nyingi ambazo zimeiwezesha kuwakopesha wakulima wengi na hatimaye kutangazwa kuwa mionghoni mwa benki kubwa nchini
Benki hiyo ndiyo imekuwa Mdhamini Mkuu wa maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoanza kesho Ijumaa kwenye viwanja vya nane nane mkoani Dodoma ambapo Makamu wa Rais Dk Philip Mpango anatarajiwa kuyatembelea.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Frank Nyabundege wakati akizungumza na waandishi wa habari ,kuhusu maonyesho hayo na udhamini wa milioni 400 wa benki hiyo kwenye maonyesho hayo.
Alisema TADB imeamua kudhamini maonyesho hayo kama sehemu ya shamra shamra za kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015 na mafanikio makubwa waliyoyapata.
Alisema TADB imefanya mambo makubwa kwenye sekta ya kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na sekta mbalimbali za serikali.
Alisema benki hiyo imeamua kudhamini maonyesho hayo kwa kuwa yenyewe ndiyo kinara wa utoaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo.
“Sisi ndiyo kinara wa mikopo ya sekta ya kilimo kwasababu tunawakopesha wakulima wengi sana na mwaka huu tumehitimu kuwa miongoni mwa benki kubwa hapa nchini,”alisema
“Benki zimewekwa kwenye makundi matatu, benki ndogo, benki za kati na kubwa sisi tulianza na mtaji mdogo lakini mwaka huu ndipo tumeingiza kuwa benki kubwa nchini baada ya mizania yetu kuzidi trilioni moja,” alisema
“Mtu anaweza kuhoji mmefikaje mbali kiasi hicho ndani ya muda mfupi wakati kuna benki zimekaa miaka zaidi ya 20 lakini bado hazijafikia kuwa benki kubwa, jibu ni kwamba tumefika hapa kutokana na utashi wa kisiasa wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akituongezea mtaji mwaka hadi mwaka,” alisema
Alisema Rais Samia alipoingia madarakani aliweka kipaumbele kuimarisha na kuboresha sekta ya kilimo na alifanya hivyo kwa kufahamu kuwa sekta hiyo ndiyo inaajiri asilimia sabini ya wakulima.
“Rais Samia alitambua kuwa ukigusa sekta ya kilimo umegusa maisha ya watanzania wengi na ndiyo sababu amekuwa kwa muda wote akiwekeza kwenye sekta ya kilimo ili kuiinua sekta hii na kuinua kipato cha watanzania,” alisema
Alisema wakati anaingia madarakani Rais Samia alikuta bajeti ya kilimo ikiwa ni bilioni 264 lakini kwenue utawala wake bajeti hiyo imepanda hadi kufikia trilioni 1.2.
“Alipoingia madarakani TADB ilikuwa na mtaji wa bilioni 60 lakini ametuongezea mtaji wa shilingi bilioni 442 na riba asilimia 20 mpaka 30 akaweka trilioni moja Benki Kuu (BoT) kama dhamana ya kuchachua uchumi ili benki za biashara zikopeshe sekta ya kilimo chini ya asilimia 10,” alisema
0 Comments