Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Saimon Siro ameripoti kuanza kazi katika kituo chake mkoani Kigoma baada ya uteuzi uliofanywa na Raisi Samia hivi ambapo amesema kuwa Diplomasia ya uchumi itakuwa moja ya vipaumbele vyake katika utekelezaji wa majukumu yake mkoani humo.
Akizungumza katika hafla ya mapokezi aliyoandaliwa na viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo Mkuu huyo wa mkoa Kigoma alisema kuwa wakati anaapishwa alipewa maelekezo kuwa mkoa Kigoma ni mkoa wa Mkakati kuchumi kwa nchi hivyo anapaswa kuuangalia vizuri mkoa huo kwenye masuala ya uchumi na biashara hivyo amelibeba suala hilo kwa uzito mkubwa.
Siro alisema kuwa mkoa Kigoma unapaka na nchi za ukanda wa maziwa makuu ambazo mkoa Kigoma una nafasi kubwa ya kutekeleza diplomasia ya uchumi hivyo kutokana na hilo ameahidi kusimamia kwa karibu kuhakikisha hilo linatekelezwa.
Akizungumzia masuala ya uchaguzi Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa alipewa maelekezo na Rais Samia kusimamia Uchaguzi uwe wa Amani, Haki na utulivu ambapo alibainisha kuwa mambo hayo hayawezi kutekelezwa bila kuwepo kwa ushirikiano wa wadau wote wa masuala ya siasa na uchaguzi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa mkoa Kigoma Mstaafu, Thobias Andengenye alisema kuwa wananchi wa mkoa Kigoma wanapenda maendeleo na wako tayari kwa hilo na kwamba uwepo wa miundo mbinu duni (barabara) na umeme usio na uhakika ulikwamisha mchakato wa maendeleo kwa mkoa huo.
Hata hivyo Andengenye alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano ambayo amekuwa Mkuu wa mkoa Kigoma serikali imetoa kiasi cha shilingi Trilioni 11.4 ambazo zimewezesha kutekelezwa kwa miradi mikubwa ikiwemo miradi ya barabara za kiwango cha lami, kuunganishwa kwenye umeme wa gridi ya Taifa na miradi mingi ya wananchi ikiwemo elimu, afya, maji na miradi ya kukuza uchumi.
Awali Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa, Zainabu Katimba alisema kuwa kwa miaka mitano ambayo Andengenye amekuwa Mkuu wa mkoa Kigoma amefanya kazi kubwa ambayo imeleta mabadiliko na maendeleo makubwa kwa mkoa huo.
0 Comments