Header Ads Widget

TAMASHA LA FILAMU KILIMANJARO 2025 LAANZA RASMI | FILAMU 100 KUONESHWA.

 


 Tamasha kubwa la filamu linalotambulika kama "Kilimanjaro Film Festival" linaendelea kufanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo pamoja na mambo mengine washiriki watashuhudia utoaji wa tuzo kwa filamu zilizoingizwa kwenye ushindani.

Tamasha hili lililoanza Jumanne Julai 2 linafanyika katika viwanja vya John Shule Park, eneo la Karanga mjini Moshi na litamalizika July 6,2025.

Muandaaji wa Tamasha hilo amesema kuwa Tamasha linahusisha zaidi ya filamu 100 bora kutoka miongoni mwa kazi zaidi ya 3,000 zilizowasilishwa kutoka nchi zaidi ya 135 duniani.

Sambamba  na hayo amesema zaidi ya filamu 3000 zimechujwa kutokanana na kutokuwa na maadili ya kitanzani.


"Ndio maana tunasisitiza kuwa wanaotengeza na wanaocheza filamu na waandishi waandike vitu ambavyo vinaendana na maadili ya Kitanzania lakini pia vinavyohamasisha mambo mazuri ikiwemo utalii ,uongozi bora ,upendo na amani kwa ujumla."alisema.

Ameendelea kusema kuwa kumekuwepo na matamasha mengi kwa zaidi ya miaka 20 yamekuwa yakifanyika katika maeneo mengi ya Tanzania lakini kwenye 

Sanaa ya filamu imesahaulika na kusema kupitia tamasha hilo itaweka historia na kumbukumbu .

" burudani ya tamasha la filamu ,muziki na matamasha mengine yapo yanafanyika ,tukasema lazima na sisi kama watu wa tasnia ya ubunifu sanaa na utamaduni tulete kitu ambacho kitakuwa na kumbukumbu katika jamii.

Amesema kuwa tamasha hilo halijalenga kutazama filamu pekee bali kutakuwepo mafunzo mbalimbali kwa wanawake vijana na watoto. 


 Tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Kilimanjaro, linawaalika wananchi wote wadau wafilamu kuweza kufika na kushuhudia burudani mbali mbali zitakazotolewa na wasanii mbali mbali, kupata elimu na pia kutoa mchango wao katika tasnia ya filamu ambayo ni moja ya fursa za kiuchumi kwa vijana hapa nchini huku takribani filamu 100 zikishuhudiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI