Header Ads Widget

RUWASA YAPELEKA NEEMA YA MAJI VIJIJI 10 VYA WILAYA YA IKUNGI


 Na Thobias Mwanakatwe,IKUNGI

WANANCHI 12,500 wa vijiji 10 katika  Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wataondoka  na kero ya ukosefu wa maji safi na salama baada ya baada Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kujenga mradi wa maji wa visima 10 ambao umegharimu Sh.milioni 896.232.


Meneja wa RUWASA Wilaya ya Ikungi, Mhandisi Shafii Shabani, akitoa taarifa leo (Julai 23, 2025) akiwa na Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida,Lucas Said baada ya Mwenge wa Uhuru kuutembelea na kuweka jiwe la msingi, amesema mradi huo ambao ujenzi wake umeanza Februari 1, 2025 unatarajia kukamilika Julai 30, mwaka huu.
 
Amesema mradi huo utakapokamilika utawanufaisha wananchi 12,500 wa vijiji vya Wibia,Damankia,Tupendane,Nkundi,Manjaru,Ufana, Kinyampembee,Jerumani,Msosa na Mwisi.


Shabani amesema visima vilivyochimbwa vina kina kuanzia mita 50 hadi 180 vikiwa na uwezo wa kuzalisha majia kuanzia lita 3,500 hadi 8,000 kwa saa.
Amesema kazi.zilizofanyika hadi sasa ni uchimbaji wa visima virefu, ujenzj wa miundombinu ya bomba za kusafirishia maji mita 15,000,ujenzi wa vioski vyenhe matenki ya plastili ya kuhifadhia maji lita 10,000 kila kijiji, ufungaji wa mfumo wa umeme wa jua na pampu ya kusukuma maji.

Ameongeza kuwa mradi huo umegharimu Sh.896,232,366.34 ambapo kazi ya hizo zilizotolewa na serikali ni Sh.890,432,366.34 na mchango wa wananchi ni Sh.5,800,000 kwa utoaji wa ardhi katika vijiji vyote 10.

Shabani amesema faida za mradi huo ni pamoja na kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji na kusogeza huduma karibu na jamii,kupunguza magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama na jumuiya ya watumiaji maji ngaji ya jamii imesaidia kusimamia utunzaji wa miradi hiyo.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi, akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo aliipongeza RUWASA kwa jinsi ambavyo imekuwa ikitekeleza miradi ya maji na kuwaondolea kero ya maji wananchi.

Amesema RUWASA wanatekeleza vyema mkakati wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan wa kumtua ndoo mama kichwani na kuwaomba wananchi kuitunza miradi ya maji inayojengwa kwenye maeneo yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI