MATUKIO DAIMA, KILOLO.
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo wametakiwa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa ajili ya kusukuma miradi ya maendeleo kukamilika kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri fedha za serikali kupelekwa kwa ajili ya miradi hiyo.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James wakati wa ziara yake ya kwanza wilayani humo, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa kujituma zaidi kwani serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitoa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maendeleo.
Alisema kuwa Halmashauri ya Kilolo imekuwa ikitumiwa vibaya na baadhi ya watumishi wake na hivyo kushindwa kusukuma miradi ya maendeleo hadi kukamilika.
“mnajua ndugu zangu halmashauri nyingine fedha za miradi zinazoletwa na serikali zinafanya kazi ya kukamilisha miradi husika ila kwa Kilolo pesa zinamalizika bila mradi kukamilika nisema ukweli katika uongozi wangu mkoni hapa sitapenda kuona Halmashauri inazidi kujitokeza na kutoa matamko ya uzembe wa kutokukamilika kwa miradi sipo tayari kuipoteza imani niliyoaminiwa na Rais wangu kabisa hilo sitaweza kukubali” alisema mkuu wamkoa Iringa Kheri Ja
Alisema kuwa hawtokubali kuona kilolo fedha zinapotea vyo na miradi isikamilike kwa uzembe wa baadhi ya watendaji na kuagiza Idara husika kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa ubora.
Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya maendeleo na fedha nyingi zimeelekezwa katika miradi hiyo na ni wajibu kwa kila mtumishi kufanya kazi kama anavyopewa majukumu.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa akiwa katika mkutano wa Hadhara mji wa Ilula alikemelea tabia ya wanawake kutojitokeza kwenye mikutano ya hadhara na badala yake kujishughulisha na biashara wakati mkutano unaendelea.
Badala ya wanawake hao kujitokeza kusikiliza hoja za maendeleo na ushauri wa serikali wao hujifungia na kuuza bidhaa.
Kutokana na hali hiyo mkuu huyo wa mkoa ameagiza viongozi wa kata na mitaa kuhakikisha kila familia inatoa mwakilishi katika mikutano hiyo kufuta dhana kuwa wanawake wa Ilula hawawezi kusababisha mabadiliko chanya.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na watu wengi alisema kuwa muda mfupi walipo kuwa wakisubiri magari yakiaziwa kupita na kufulanya Halmashauri hiyo kuwa kimbilio.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa akiwa katika mkutano wa Hadhara mji wa Ilula alikemelea tabia ya wanawake kutojitokeza kwenye mikutano ya hadhara na badala ya kujishughulisha na biashara wakati mkutano unaendelea akisema sita kuwa viongozi kujitokeza kwenye mikutano hiyo bila ya kupiga kura wao ni sawa na kujiweka katika mazingira ya kushindwa uchaguzi.
Katika mkutano huo mkuu huyo wa mkoa ameagiza viongozi wa kata na mitaa kuhakikisha kila familia inatoa mwakilishi katika mikutano hiyo kufuta dhana kuwa wanawake wa Ilula hawawezi kusababisha mabadiliko chanya.
Alisema kuwa Halmashauri ya Kilolo imekuwa ikitumiwa vibaya na baadhi ya watumishi wake na hivyo kushindwa kusukuma miradi ya maendeleo hadi kukamilika.
0 Comments