Header Ads Widget

HALMASHAURI YA MJI MAFINGA MNAFANYA VIZURI SANA KATIKA MAKUSANYO YA MAPATO -RC KHERI JAMES

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA ,MAFINGA

MKUU wa mkoa wa Iringa Kheri James ameipongeza Halmashauri ya Mji Mafinga chini ya mkurugenzi wake Fidelika Myovela kwa kazi nzuri ya ukusanyaji mapato.

Kuwa Halmashauri hiyo imefanya kazi kubwa ya ukusanyaji mapato na inastahili pongezi na chanji inabaki .

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Mafinga leo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha toka alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Iriinga.

Alisema Halmashauri hiyo imeonesha mfano katika mapato na kuitaka kuelekeza kasi hiyo katika usimamizi bora wa fedha zinazokusanywa.

Hata hivyo alitaka watumishi wa umma kujemga utamaduni wa kushuka chini kwa wananchi ili kusikiliza kero zao na kuzitatua.


Alisema kupitia ziara hizo zitaangazia kasi ya utoaji wa huduma kwa wananchi pia kuangalia miradi iliyojengwa na serikali inawahudumiaji wananchi maana inawezakuwa miradi mizuri huduma mbaya.

Kheri aliagiza pia watumishi wa Halmashauri kujenga utaduni wa kufuatilia maagizo yanayotolewa na viongozi wa serikali ngazi za juu.

Pia aliagiza Halmashauri kuweka utatatibu mzuri wa kupanga matumizi bora ya ardhi na kusimamia mipango hiyo .


 Akizubgumzia kuhusu maadili ya watumishi mkuu huyo wa mkoa aliwataka watumishi wa umma kuhakikisha wanakuwa na maadili mema kazini na uraiani ili kuiheshimisha serikali.

Alisema kuwa mtumishi wa umma huzuiwi kuwa na faragha zako na starehe zako ila pale zipopozidi kwa kujiachia ni vema kuwa na staha badala ya kufanya mambo yanayochafua serikali.

Alisema kuwa maisha binafsi ya mtumishi yasiichafue serikali hivyo lazima faragha za kila mmoja zifanyike kwa kulinda heshima ya mtumishi mwenyewe na serikali .

Kheri alisema suala la uaminifu kwa watumishi ni jambo la muhimu kwani iwapo mtumisha atakuwa mwaminifu atafanya wananchi kuendelea kuwa na imani na Watumishi na Halmashauri.

Alisema kuwa fedha za miradi zinapoletwa na serikali fedha hizo zitumike kwa malengo yaliyopangwa na isiwe pesa za serikali za miradi kutumika kujenga nyumba binafsi za watumishi.

"kuna watumishi wasio waaminifu fedha za ujenzi wa zahanati ama kituo cha afya zinapoletwa na yeye siku hiyo hiyo anaanza ujenzi wa nyumba yake binafsi hili si sawa"

Alisema wananchi wanategemea serikali kuboresha huduma zao hivyo lazima watumishi kuwa na mapokezi mazuri kwa wananchi na kutoa huduma bora ili kila mwananchi aone furaha ya kuhudumiwa na serikali.


Akisoma taarifa ya Halmashauri hiyo mbele ya mkuu wa mkoa mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Fidelika Myovela alisema kuwa hadi kufikia  juni 30 mwaka huu Halmashauri hiyo imekusanya jumla ya shilingi 8,019,473,055.62 ambayo ni sawa na asilimia 120 ya lengo la makusanyo ya mwaka 2024/2025 ambayo ni shilingi 6,676,760.83 

Kuwa kati ya fedha hizo zilizokusanywa mapato Halisi ni shilingi 5,584,032.54 sawa na asilimia 121 na mapato fungwa ni shilingi 2,435,440,575.08 sawa na asilimia 118.

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na makusanyo hayo Halmashauri ya Mji Mafinga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ilikisia kutumia kutoka vyanzo mbali mbali vyenye jumla ya shilingi 31,916,837,363.83 .

Aidha Halmashauri hiyo hadi kufikia  mwezi Juni 2025 imefanikiwa kutumia jumla ya shilingi 28,911,732,831.04 ambazo ni ya miezi 12 ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka ambayo ni sawa na asilimia 95.55 ya fedha zilizokusanyea na kupokelewa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI