Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump amemshutumu rais wa zamani Barack Obama kwa "uhaini," akidai alipanga kuhujumu muhula wake wa kwanza wa urais kwa kumhusisha na madai ya Urusi kuingilia uchaguzi mkuu.
"Walijaribu kuiba uchaguzi," Trump alisema katika Ikulu ya White House akidai Obama alitaka kuhujumu ushindi wake wa uchaguzi wa mwaka 2016 dhidi ya Hillary Clinton.
Msemaji wa Obama amejibu tuhuma hizo, akiliita shambulio la Trump "jaribio dhaifu la kuwavuruga watu."
Trump alinukuu ripoti kutoka kwa Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani, Tulsi Gabbard wiki iliyopita ambayo inamshutumu Obama na timu yake ya usalama wa taifa kwa kuandaa "mapinduzi ya dhidi ya Rais Trump" - ripoti ambayo chama cha Democrats kimesema ni ya uwongo.
Maoni ya Trump ya Jumanne yalikuja wakati akikabiliwa na maswali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mnyanyasaji wa kingono marehemu Jeffrey Epstein, ambaye alijiua gerezani 2019 akisubiri kesi.
Utawala wa Trump umekuwa chini ya shinikizo kutoa habari zaidi kuhusu Epstein.
0 Comments