Header Ads Widget

"HATUTAKI VITA ILA TUKO TAYARI KUISHAMBULIA ISRAEL"- IRAN

Rais wa Iran Masoud Pezzekian amesema kuwa vikosi vya jeshi vya nchi hiyo viko tayari "kushambulia ndani kabisa ya Israel".

Akizungumza na Al Jazeera siku ya Jumanne, Julai 22, Bw. Pezzekian alisisitiza kwamba kutilia maanani mpango wa nyuklia wa Iran kuwa umekamilika ni kitu cha "kufikirika" kwa sababu, kwa maoni yake, mpango wa nyuklia wa Iran uko "katika akili za wanasayansi wa nchi hiyo "na sio kwenye "vituo vya nyuklia".

Kwa mara nyingine alisisitiza misimamo ya nchi yake kuhusu haki ya kurutubisha madini ya uranium na mpango wa nyuklia.

Rais wa Iran aliiambia Al Jazeera: "Israeli imetushambulia," lakini Iran pia "imeshambulia Israeli kwa nguvu kubwa," ingawa, kulingana na Bw. Pezzekian, Israeli "haitangazi" uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Iran.

Bw. Pezzekian pia alisema kuwa sababu kuu ya "kuingiliwa kijasusi" katika ngazi za juu zaidi za kijeshi za nchi hiyo, ambayo pia anakubali, ni kutokana na matumizi ya Israeli ya "teknolojia na uwezo wa Marekani".

Haya ni mazungumzo ya kwanza kati ya Rais wa Iran na Al Jazeera baada ya shambulio la kombora la nchi hiyo kwenye kambi ya Marekani ya Udeid nje kidogo ya mji wa Doha, na kuhusiana na hilo, Bw. Pezzekian kwa mara nyingine alisisitiza msimamo wa nchi yake kwamba "Iran haikuwa na nia ya kuishambulia Qatar."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI