Na,Jusline Marco Arusha.
Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi eneo la Ngorongoro NCAA Abdul-Razaq Badru ameongoza Maafisa na askari wa Mamlaka hiyo katika zoezi la upandaji miti kwenye Shule ya Sekondari Welweli,ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira kwa wanananchi katika hitimisho la Maadhimisho ya Siku ya Askari Wanyamapori Duniani.
Katika hitimisho hilo Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro NCAA imeweza kufanya michezo mbalimbali iliyohususu askari wa Jeshi la Uhifadhi, askari wa Jeshi la polisi wilaya ya Karatu pamoja na kukimbia mbio za kilomita tano.
Kamishna Badru ameeleza kuwa NCAA ina jukumu la kutoa elimu ya mazingira na uhifadhi shirikishi kwa jamii zinazozunguka hifadhi ya Ngorongoro, hivyo katika kuadhimisha siku ya askari wa Wanyamapori, NCAA imetoaa miti bure kwa wananchi ili waweze kuipanda katika maeneo yao ambapo ametumia fursa hiyo kuzungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo na kuwasisitiza utunzaji wa miti iliyopandwa pamoja na mazingira kwa ujumla."NCAA ni sehemu ya Jamii, katika utekelezaji wa majukumu yetu tunashirikiana na vyombo vingine ikiwepo Polisi Wilaya za Ngorongoro na karatu pamoja na wananchi, ndio maana leo tumefanya michezo ya riadha, mazoezi yaa viungo, mchezo wa mpira wa miguu ili kuendelea kutuweka pamoja hasa katika shughuli za kuimarisha usalama na ulinzi wa rasilimali za Nchi) alifafanua Kamaishna Badru.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu, katika Maadhimisho hayo Katibu tawala wa Wilaya ya Karatu Bw. Bahati Mfungo ameipongeza NCAA kwa ushirikiano inaoutoa kwa wananchi wa Wilaya hiyo hasa kwa kuwapa elimu ya mazingira, upandaji miti, kupambana na mgongano kati ya Wanyamapori na wananchi pamoja na kusaidia miradi mbalimbali ya wananchi ikiwemo huduma za kijamii.
Siku ya Askari wa Wanyamapori Duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 2007 kwa lengo la kuwakumbuka askari waliopoteza maisha wakati wa itekelezaji wa majukumu yao,ambapo kauli mbiu ya maashimisho ya mwaka huu ni “ Walinzi:Kuimarisha uhifadhi wa Mabadiliko" ikiwa imelenga kuutambua mchango wa askari wa Wanyamapori katika kuleta mabadiliko ya kweli kwenye uhifadhi wa maliasili ambayo ni urithi wa Taifa.
0 Comments