Header Ads Widget

MWANDISHI WA UHURU NA MZALENDO LATIFA GANZEL AONGOZA KURA ZA MAONI UDIWANI UWT MOROGORO MJINI

NA MATUKIO DAIMA MEDIA MOROGORO

🌍Sura mpya ndani ya siasa za UWT Manispaa ya Morogoro zashika kasi


🌍Vigogo watatu wa zamani kati ya wanne waliotetea nafasi zao waangushwa

Morogoro Mjini imeshuhudia historia mpya katika siasa za wanawake ndani ya CCM baada ya Uchaguzi wa UWT wa kura za maoni kutafuta watakaopeperusha bendera ya udiwani wa viti maalum katika manispaa ya Morogoro kukesha usiku na mchana  kwenye kupiga, kuhesabu kura Hadi kutangazwa matokeo siku ya pili.

Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM, UVCCM manispaa ya Morogoro Khalid King, jumla ya wanawake 1,155 kutoka kata 29 za manispaa ya Morogoro waliojitokeza kupiga kura, kati yake kura 29 ziliharibika na hivyo kura halali kubaki 1,124 kwa wajumbe wa kata 29 za manispaa hiyo 

Mwandishi wa habari wa Uhuru na Mzalendo wa Mkoa wa Morogoro Bi.Latifa Said Ganzel,ameibuka na kura nyingi zaidi kuliko wenzake kwenye uchaguzi huo wa madiwani wa viti maalum kupitia UWT.

Latifa alipata kura 934 akifuatiwa na Batuli Kifea (794), Grace Mkumbae (752), Salma Mbandu, Imakulata Mhagama, Warda Bazia Rahma Maumba Magreth Ndewe, Anna Kisimbo na Amina Zihuye waliongoza na kuwa ndani ya nafasi ya kumi za juu kati ya wagombea 31 waliowania nafasi hizo.

Uchaguzi huo umeibua hamasa kubwa hasa miongoni mwa Wanawake wachanga katika Uongozi mbao walishiriki kwa ari na uwajibikaji mkubwa kutoka kata na matawi kwenye kata 29 za manispaa ya Morogoro.

Wachambuzi wa kisiasa ndani ya Manispaa ya Morogoro wameutafsiri ushindi huo kuwa ni mwanzo wa sura mpya ndani ya siasa za wanawake baada ya Vigogo watatu waliotumikia miongo kadhaa ya udiwani na waliokuwa na ushawishi kutopenya ndani ya 10 Bora.

 "Hii ni sura ya uwezo na hoja, si jina wala sifa za nyuma pekee"Alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka kutambulishwa jina lake  majira ya saa 12 kasoro asubuhi alipoona Vigogo hao wakiondoka ukumbini walikofungiwa muda mrefu kwenye zoezi la kuhesabu kura.

Baadhi ya walioshindwa kupenya 10 Bora  ni pamoja na  Mama Nyau (Hadija Kibati), Zamoyoni Abdallah, Mwanaidi Ngulungu na mwingine Aisha Kitime jambo lililozua mijadala mizito mitandaoni kuhusu kuhitajika kwa mabadiliko ya uongozi ndani ya UWT.

“Wanawake wa Morogoro wameonyesha wanatamani sura mpya, hoja mpya, nguvu mpya, wakipita Hawa tuwapime kwa uwezo na utendaji wao,” Alisema mmoja wa wajumbe Joyce Hendrick.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI