Header Ads Widget

ASILIMIA 70 YA WANAFUNZI WA KIKE WALIOKATISHA MASOMO WAREJEA SHULENI GEITA

 


Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema kuwa tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan la kuwataka watoto wa kike waliokatisha masomo kwa sababu ya ujauzito kurejea mashuleni limetekelezwa ipasavyo ambapo kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025 zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi hao wamerejea kuendelea na masomo yao

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita Shigela amesema hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa mtoto wa kike kwani imewapa fursa ya pili kutimiza ndoto zao na kujenga maisha yao kupitia elimu

"Kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto wa kike katika shule mbalimbali hali inayoonesha mwitikio chanya wa jamii na mafanikio ya utekelezaji wa sera hiyo ya kitaifa ambapo serikali ya mkoa inaendelea kuhakikisha hakuna mtoto wa kike anayeachwa nyuma katika upatikanaji wa elimu, " Amesema.


 Katika kuelezea mafanikio ya sekta ya elimu Shigela amesema utekelezaji wa mpango wa elimu bila ada umeendelea kuimarika ambapo serikali imeongeza bajeti kutoka shilingi bilioni 6 nukta 4 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 19 nukta 9 mwaka 2025 hatua ambayo imerahisisha upatikanaji wa elimu kuanzia ngazi ya awali hadi kidato cha sita

Amesema kuwa idadi ya shule za msingi na awali imeongezeka kutoka shule 641 mwaka 2021 hadi shule 792 mwaka 2025 huku shule za sekondari zikiongezeka kutoka 130 hadi 240 katika kipindi hicho ambapo vyumba vya madarasa vimeongezeka kutoka 7206 hadi 10540 na nyumba za walimu zimeongezeka kutoka 2272 hadi 2375

Aidha uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo elimu ya awali imefikia wanafunzi 227087 mwaka 2025 kutoka wanafunzi 73446 mwaka 2021 darasa la kwanza kutoka 107519 hadi 334224 kidato cha kwanza kutoka 37834 hadi 131645 na kidato cha tano kutoka wanafunzi 1900 hadi 2618.


"Kwa upande wa ufaulu wanafunzi wa darasa la saba wamefaulu kwa asilimia 71 nukta 53 mwaka 2024 ikilinganishwa na asilimia 82 nukta 49 mwaka 2021 huku ufaulu wa kidato cha nne ukifikia asilimia 94 nukta 45 mwaka 2024 kutoka asilimia 84 nukta 56 mwaka 2021 na kidato cha sita ukibaki juu kwa wastani wa asilimia 99 kwa miaka yote, " Amesema Mkuu huyo. 

Amesema idadi ya walimu imeongezeka kutoka 8876 hadi 9156 kwa elimu ya msingi na kutoka 3398 hadi 3696 kwa elimu ya sekondari ambapo serikali pia imekamilisha ujenzi wa vyuo vya kati vya VETA kutoka kimoja mwaka 2021 hadi vitano mwaka 2025 na vyumba vya maabara kutoka 165 hadi 338

Shigela ameongeza kuwa mabweni 74 ya wasichana mabwalo 19 hosteli tano majengo ya utawala 12 na matundu ya vyoo 14133 yamekamilika katika shule mbalimbali hali iliyoboreshwa mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wote hususan watoto wa kike

Amesema pia wanafunzi wa MEMKWA wameongezeka kutoka 2169 hadi 2269 na wanafunzi wenye mahitaji maalum wameongezeka kutoka 1052 hadi 2233 hatua ambayo inaonesha juhudi za serikali katika kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote bila ubaguzi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI