Header Ads Widget

MKUTANO WA PILI WA MABARAZA YA HABARI AFRIKA 2025 WAFUNGUA FURSA MPYA ZA MAGEUZI YA VYOMBO VYA HABARI

 


Na Pamela Mollel, Arusha

Mkutano wa pili wa Mabaraza ya Habari Afrika 2025 umeelezwa kuwa ni fursa ya kihistoria kwa vyombo vya habari barani Afrika kuimarisha ushirikiano, kukuza teknolojia na kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya sekta ya habari.

Akizungumza Julai 14, 2025 jijini Arusha, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, amesema kuwa Tanzania kupitia MCT inaongoza juhudi za kuleta mageuzi ya vyombo vya habari na matumizi ya teknolojia ya kisasa ili kukuza uhuru wa habari na weledi wa tasnia hiyo.

“Mkutano huu ni hatua muhimu kwa Afrika katika kujadili kwa pamoja namna bora ya kuimarisha tasnia ya habari, hasa katika kipindi hiki cha mageuzi ya kidigitali,” alisema Sungura.


Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano na Habari kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Dkt. Tawfik Jelassi, ametoa wito kwa vyombo vya habari barani Afrika kuongeza juhudi katika kusimamia utekelezaji wa sheria na sera zilizowekwa kwa lengo la kulinda uhuru wa vyombo vya habari na uwajibikaji.

Mkutano huo umehusisha wadau kutoka mabaraza mbalimbali ya habari barani Afrika na mashirika ya kimataifa, huku ajenda kuu ikiwa ni kuboresha mazingira ya kazi kwa wanahabari na kuhakikisha vyombo vya habari vinakuwa sehemu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI