Header Ads Widget

MACRON KULITAMBUA TAIFA LA PALESTINA

 


Rais Emmanuel Macron amesema Ufaransa italitambua rasmi taifa la Palestina mwezi Septemba jambo ambalo litalifanya kuwa taifa la kwanza la G7 kufanya hivyo.

"Lenye uhitaji mkubwa hii leo ni kukomeshwa kwa vita huko Gaza na raia waokolewe. Amani inawezekana kufikiwa. Tunahitaji usitishaji mapigano mara moja, kuachiliwa kwa mateka wote, na msaada mkubwa wa kibinadamu kwa watu wa Gaza," aliandika.

Maafisa wa Palestina walifurahishwa na uamuzi wa Macron, huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akisema hatua hiyo "inaunga mkono ugaidi" kufuatia shambulio la Hamas la tarehe 7 Oktoba 2023 nchini Israel.

Katika chapisho lake kwenye ntandai wa X siku ya Alhamisi, Macron aliandika: "Mkweli kwa ahadi yake ya kihistoria kwa haki na amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati, nimeamua kuwa Ufaransa itatambua Jimbo la Palestina.

"Lazima pia tuhakikishe kuondolewa kwa Hamas, na kulinda na kuijenga upya Gaza.

"Mwishowe, ni lazima tujenge Taifa la Palestina, tuhakikishe uwepo wake, na pia kuhakikisha kwa kukubali kuondolewa kwa jeshi na kuitambua kikamilifu Israel, kunachangia usalama wa wote Mashariki ya Kati. Hakuna njia mbadala."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI