Ujio wa kampeni ya “Chupa la Machupa, Utamu Ndani ya Chupa” kutoka Coca-Cola umeibua ari mpya miongoni mwa vijana na akinamama wafanyabiashara wadogo, huku wengi wakiiita kampeni hiyo kuwa ni yenye ladha ya mafanikio.
Katika mtaa wa Sabasaba, Kingolwira na maeneo ya Msamvu, ni kawaida sasa kuona watu wakifungua soda kwa hamasa wakisubiri ujumbe wa zawadi ndani ya chupa tangu kuanza kwa kampeni hii.
Biashara za mama lishe, vibanda vya vyakula na wauzaji wa vinywaji baridi zimeongezeka kasi ya mauzo.
“Mteja akinunua soda anasema ‘Naomba ya zawadi!’ Hii inaonyesha promosheni si ya kawaida. Imetujengea uaminifu na imetusaidia kuongeza mauzo,” alisema Jumanne Haji, kijana msambazaji wa soda.
Kampeni hiyo, mbali na kutoa zawadi zikiwemo soda za Bure na pesa taslimu, imeibua ushawishi wa kibiashara unaochochea mzunguko wa fedha katika mitaa ya Morogoro.
Meneja Mauzo wa Coca-Cola kanda ya Morogoro, Nelson Andrew alisema:
“Hii ni zaidi ya promosheni – ni ushirikiano wa kweli kati ya Coca-Cola na jamii ya wafanyabiashara wadogo. Lengo ni kukuza kipato chao, kuboresha maisha yao na kusaidia ndoto zao.”Alisema
Mmoja wa wafanyabiashara wa jumla Mussa Erasto na Mjasiriamali Tumaini Kamwela walisema kampeni hiyo imeongeza fursa nyingi za kibiashara sambamba na ongezeko la mauzo.
0 Comments