Header Ads Widget

ISRAEL NA MAREKANI ZAJIONDOA KATIKA MAZUNGUMZO YA KUSITISHA MAPIGANO GAZA NCHINI QATAR

 

Wapatanishi wa Israel na Marekani wameamua kuondoka katika mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza katika mji mkuu wa Qatar Doha, huku Washington ikiishutumu Hamas kwa "kutotenda kwa nia njema".

Katika taarifa yake, mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff alisema: "Tumeamua kuirejesha timu yetu nyumbani kutoka Doha kwa mashauriano baada ya majibu ya hivi punde kutoka kwa Hamas, ambayo yanaonyesha wazi kutokuwa na nia ya kufikia usitishaji vita huko Gaza."

Serikali ya Israel haikusema ni nini kiliichochea kujiondoa kwake, lakini afisa mmoja mkuu wa Israel alinukuliwa katika vyombo vya habari vya ndani akisema hakuna "kuvunjika" katika mazungumzo hayo.

Hamas ilisema imeshangazwa na matamshi ya Witkoff na kwamba ina nia ya kuendelea na mazungumzo.

Pande zote zinazohusika katika mazungumzo hayo - ikiwa ni pamoja na wapatanishi - zinakubali kwamba mapungufu makubwa yanasalia katika masuala muhimu.

Katika taarifa ya Alhamisi, Witkoff alisema kuwa "wakati wapatanishi wamefanya juhudi kubwa, Hamas haionekani kuwa na uratibu au kutenda kwa nia njema".

"Sasa tutazingatia chaguzi mbadala za kuwarudisha mateka nyumbani na kujaribu kuunda mazingira ya utulivu zaidi kwa watu wa Gaza.

"Ni aibu kwamba Hamas imetenda kwa njia hii ya ubinafsi. Tuna dhamira ya dhati katika kutafuta kumalizika kwa mzozo huu na amani ya kudumu huko Gaza."

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI