Header Ads Widget

CHAVALA YOHANNES MATONYA AJA NA VIPAUMBELE VYA TUMAINI MAPYA KWA JIMBO LA MUFINDI KUSINI

Na Matukio Daima Media  Mufindi

WAKATI mchakato wa kura za maoni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ukiendelea ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM ) kwa wagombea ubunge kuendelea kujinadi kwa wajumbe  jina la Chavala Yohannes Mayonya limeendelea kuvuma kama mmoja wa vijana wenye dira, maono na mapenzi ya dhati kwa maendeleo ya wananchi wa Mufindi Kusini.

Matonya, ambaye ni kada wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameibuka kuwa tumaini jipya kwa wakazi wa jimbo hilo kutokana na ajenda zake mahususi zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi.

Miongoni mwa mambo anayoyapa kipaumbele ni kuimarisha mawasiliano na miundombinu ya teknolojia katika maeneo ya vijijini, hasa kwenye vituo vya afya, mashule na ofisi za kata za Serikali pamoja na CCM. 


Pia Matonya anasema kuwa maeneo mengi ya Mufindi Kusini bado hayajafikiwa na huduma bora za mawasiliano ya kisasa, hali inayokwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

"Kama taifa tunapoelekea kwenye uchumi wa kidigitali, hatuwezi kuwaachwa nyuma watu wa Mufindi Kusini tuna wajibu wa kuhakikisha tunaleta mawasiliano ya uhakika kwenye kila kituo cha huduma kwa jamii," anasisitiza Matonya.

Mbali na suala la mawasiliano, Matonya ameweka mkazo mkubwa katika uboreshaji wa huduma za afya. 

pia alisema  kuwa bado vituo vingi vya afya katika jimbo hilo vinakabiliwa na uhaba wa dawa, vifaa tiba na watumishi wenye sifa stahiki. 

Anaamini  kuwa kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo, hali hiyo inaweza kubadilishwa kwa haraka.

Aidha, Matonya ametaja barabara kuu ya kiuchumi inayopita Mafinga – Zero Zero – Mtwango – Mgololo – Nyigo kama uti wa mgongo wa maendeleo ya Mufindi. 

Anasema kuwa barabara hiyo inahitaji maboresho makubwa ili kuimarisha usafirishaji wa mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani. 

Pia amesisitiza umuhimu wa kuboresha barabara ya kutoka Ziro Zeio – Mtwango kwenda Lufuna, Kibao, Lugoda, Mninga, Igowole hadi Nyololo ili kuunganisha kata na vijiji vingi vinavyotegemea kilimo kama njia kuu ya uchumi.


Matonya ameeleza azma yake ya kusimamia kwa karibu uboreshaji wa miundombinu ya elimu, hasa madarasa ya mashule ya msingi na sekondari pamoja na vituo vya afya chakavu. 

"Madarasa yaliyotengenezwa miaka ya nyuma yamechakaa mno tunahitaji kujenga mazingira rafiki kwa wanafunzi na walimu wetu hii ni msingi wa mustakabali wa kizazi kijacho," amesisitiza.

kwa vipaumbele hivi ambavyo amekuwa akijinasibu ni wazi  Chavala Yohannes Matonya anajipambanua kama kiongozi anayegusa nyanja muhimu zinazolenga kuinua maisha ya wananchi wa Mufindi Kusini. 

kwani kauli mbiu yake ya maendeleo jumuishi, inaendelea kuwavuta wakazi wengi wa jimbo hilo ambao wanaamini kuwa ni wakati wa kupata kiongozi mwenye maono mapana, usikivu na uwajibikaji wa kweli.


Alisema atahakikisha anadumisha upendo na mshikamano wa Wanamufindi wote bila kubaguana kwa namna yoyote ile Ubaguzi wa aina yoyote ile ni dhambi mbele ya Mungu wetu mwema.

Pia kuhakikisha anashirikiana na Viongozi wetu wa Chama, Serikali , Taasisi za dini na taasisi zote zilizopo na nitakazo ziongeza ndani ya Mufindi Kusini yetu.


Hata hivyo alisema ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi mpya za Kata za Serikali na Chama- CCM ili zifanane na hadhi ya Wanauchumi Wananchi wa Mufindi .

Ikumbukwe kuwa macho na masikio ya wengi sasa ni kwenye  vuguvugu la uchaguzi ndani ya CCM ambalo limezidi kushika kasi, huku macho na masikio ya wakazi wa Mufindi Kusini sasa yameelekezwa kwa Matonya, kijana mwenye ari ya kuleta mageuzi chanya ya maendeleo katika nyanja zote muhimu za kijamii na kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI