Waziri wa Ulinzi wa Israel ameonya kuwa wakazi wa Tehran "watalipia gharama" ya mashambulizi ya Iran dhidi ya raia wa Israel baada ya mashambulizi ya usiku kusababisha vifo vya watu watano na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Israel Katz alimshutumu kiongozi wa Iran Ali Khamenei kwa kulenga maeneo ya kiraia kwa makusudi "ili kuwazuia IDF kuendelea na mashambulizi ambayo yanaporomosha uwezo wake."
Katz alimwita Khamenei "muuaji muoga" na "dikteta mwenye majivuno". Alisema Israel italipiza kisasi "hivi karibuni".
0 Comments