Shirika la kijasusi la Uingereza, maarufu MI6 litaongozwa na mwanamke kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 116 ya uhai wake.
Blaise Metreweli, aliyejiunga shirika hilo mwaka 1999, atakuwa mkuu wa 18 akichukua nafasi ya Sir Richard Moore baadaye mwaka huu.
Kwa sasa anahusika na teknolojia na uvumbuzi ndani ni ya shirika hilo na amesema anaona fahari na heshima kubwa kwa kupata nafasi hiyo ya uongozi.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer ameuita uteuzi huo kuwa wa kihistoria.
MI6 ina jukumu la kupata taarifa kimataifa na kuimarisha usalama wa Uingereza, kuzuia ugaidi, na kuimarisha usalama wa mtandaoni.
Mkuu wake ambaye hutambulika kwa herufi ‘C’, ndiye mtu pekee anayefahamika kwa jina mbele ya umma.
0 Comments