Header Ads Widget

WAIRAN WANAHOJI YUKO WAPI KIONGOZI WAO KHAMENEI

 Huku serikali ya Iran ikishiriki katika moja ya makabiliano makali na hatari zaidi ya kijeshi dhidi ya Israel, Ayatollah Ali Khamenei, kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hajajitokeza hadharani kwa zaidi ya wiki moja, akijificha kwa umma na hata kwa viongozi.

Kupotea kwake hwa umma kumeongeza uvumi ndani na nje ya Iran kuhusu nafasi yake kama kiongozi mkuu wa nchi na kamanda mkuu wa majeshi.

Kutolewa kwa ujumbe wake wa kwanza wa video baada ya kusitishwa kwa mapigano na Israel, baada ya siku chache tu za ukimya kamili, kulikusudia kuondoa mashaka haya, lakini badala yake sio tu kulishindwa kujibu maswali yote, bali pia kuliibua maswahili mengi kumhusu.

Kimya wakati wa vita vya kinyume na usitishaji mapigano

Dalili za kwanza za hali isiyo ya kawaida ya Ayatollah Khamenei zilianza Juni 18, siku ambayo alitoa onyo kali kwa Marekani katika ujumbe wa video aliotumwa kutoka eneo la siri na kukataa wito wa Donald Trump wa kujisalimisha bila masharti kwa Iran.

Ujumbe huo uliambatana na picha moja ambayo ni tofauti na mtindo wa hapo awali wa ofisi ya Kiongozi Mkuu, ambayo inarusha picha zake tofauti. Kwa upande mwingine, ujumbe wa sauti una marudio, ambayo yalisababisha shaka kuwa ulirekodiwa katika eneo lisilojulikana, kama kambi.

Mnamo tarehe 26 Juni, baada ya wiki moja ya ukimya kamili, Ayatollah Khamenei alionekana tena katika ujumbe wa video. Wakati huu, sura yake ilionekana kutoka upande mmoja. Mada ya ujumbe huo ilikuwa "ushindi juu ya Israeli," wakati aliepuka kutumia maneno kama "kusimamisha vita" au "makubaliano" na badala yake alitumia hadithi ya ushindi.

Mchambuzi mmoja kwenye tovuti alisema, "Wale walio karibu na [Khamenei] wanasema kwamba hali yake ya kiakili ni mbaya na wamemuondoa katika mchakato wa kufanya maamuzi... Mtazamo sasa ni juu ya nani anayeweza kuchukua nafasi yake, kwasababu yeye ni wenye msimamo mkali, na anachukua njia tofauti."

Kutokuwepo kwa Khamenei katika kilele cha mzozo huo ni ujumbe unaoweza kuashiria shaka juu ya hadhi ya kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI