Rais wa Marekani Donald Trump, amezungumza na waandishi wa habari kwenye ndege ya Air Force One.
Trump anasema hatafuti usitishaji mapigano, lakini "tunaangalia kilicho bora zaidi kuliko usitishaji mapigano".
Alipoulizwa ni kitu gani bora kuliko usitishaji mapigano, alisema: "Mwisho kabisa wa hili. Sio usitishaji mapigano. Mwisho."
Trump anasema hajawasiliana na Iran kwa mazungumzo ya amani
Katika jukwaa lake la Truth Social platform, Trump ameandika kwamba hajawasiliana na Iran kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano "kwa namna yoyote ile".
Rais wa Marekani ameongeza kuwa Iran ilipaswa kutia saini makubaliano ambayo aliweka wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Anaandika: "Hizi ni HABARI ZA UZUSHI ZAIDI, ZA UWONGO! Ikiwa wanataka kuzungumza, wanajua jinsi ya kunifikia. Walipaswa kutia Saini makubaliano yaliyokuwa mezani - Ingeokoa maisha ya mengi!!!"
0 Comments