Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema kwamba iwapo Marekani itahusika katika mzozo wa Israel na Iran, "bila shaka italiingiza eneo hilo kwenye mzozo mpana na ambao haupo kwa maslahi ya mtu yeyote".
Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamefanya mkutano leo kujadili hali ya Mashariki ya Kati. Kallas alisema kuwa nchi zote wanachama wa EU "zinakubali kwamba Iran haiwezi kuwa na bomu la nyuklia, na hilo ndilo lengo la mwisho".
Kuna maoni tofauti juu ya mpango wa nyuklia wa Iran miongoni mwa nchi wanachama. "Tunaweza kufanya nini ili kukomesha hali inayoendelea kwa sasa? EU ina jukumu la kutekeleza, nilizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Iran jana na tunakubali kuwa suluhisho la mgogoro huo ni diplomasia. Utulivu wa kanda ndio kipaumbele kwa kila mtu," alisema.
0 Comments