Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA WELEDI,KUENDANA NA SOKO LA USHINDANI

 


Na Matukio Daima Media,Morogoro 

WAANDISHI wa habari wanawake nchini wanatakiwa kuhakikisha wanafanyakazi zao kwa weledi ili kuendana na soko la ushindani hasa katika kipindi hiki cha uwepo wa ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ulimwenguni kwa kumiliki vyombo vya habari vya mtandaoni kama ilivyo kwa waandishi wanahabari wanaume.


Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja was Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), Kenneth Simbaya alisema hayo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Waandishi wa Habari wanawake ya usalama mtandaoni na kupambana na ukatili wa kijinsia mtandaoni yanayolenga kuwajengea uwezo wa kujilinda kwa kutumia njia mbadala.


Simbaya alisema ili kuendana na mazingira ya sasa ambayo teknolojia inaruhusu kazi ya uandishi wa habari kufanywa popote kutokana na uwepo wa akili unde (Mnemba).


“Sekta ya mawasiliano imekua kwa kasi kubwa kwa kuwa taarifa nyingi za kimaendeleo zinapatikana mtandaoni tofauti na miaka 20 iliyopita na jamii imekuwa ikitegemea zaidi kusoma na kupata taarifa kupitia magazeti.alisema Simbaya.


Aliongeza kwa kusema kuwa hakuna anayepinga kwamba ulimwengu sasa kila kitu kinakwenda mtandaoni na leo mnapewa mafunzo haya kwa sabsbu ulimwengu wote unakwenda huko, kama Umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania wanao jukumu kubwa katika kuhakikisha kunafanyika kila linalowezekana kwamba waandishi na klabu hazibaki nyuma na zinaendana na kasi ya maendeleo.


Simbaya alisema teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya internet ilipoingia ilikumbana na fikra kinzani kwamba kutokana na baadhi ya watu waliingiwa na hofu juu ya matumizi ya internet lakini kwa sasa internet imekuwa ni njia wezeshi ya kurahisisha upashanaji wa taarifa na maarifa katika sekta ya kibenki kwamba suala la kutoa kupokea na kutuma fedha imerahishwa kwa kiasi kikubwa.



Mwenyekiti wa Kamati ya fedha na mjumbe wa Bodi ya UTPC Lilian Lucas alisema mafunzo hayo yamejumuisha waandisbi wa habari wanawake kutoka mikoa 25 yakilenga kutambua changamoto za ukatili wa kijinsia mtandaoni na usalama mtandaoni kwa wanawake na watoto wakike ikiwa ni tishio kwa uhuru wa vyombo vya habari, kuvunja heshima ya wanawake na wasichana na ushiriki wao katika demokrasia nchini.


Lilian alisema kuwa UTPC  inajukumu la kuwawezesha waandishi wa habari wanawake kuwa na maarifa juu ya usalama wa kidigitali au mtandaoni si hiari bali ni lazima hasa ikizingatiwa ya kuwa ulimwengu mambo mengi ni mtandaoni na ujio wa akili mnemba kunafanya uwezeshaji.


“Mafunzo haya hajalengwa tu kutoa maarifa bali kuwapa uwezo ili kuweze kuwasha moto wa mabadiliko tunapaswa kuonyesha matokeo jinsi mafunzo kama haya yanavyobadilisha maisha yetu na fikra zetu na uripoti wetu baada ya mafunzo unavyobadilisha maisha ya watu sera na sheria mbalimbali kwa kufanya uandishi wa habari wenye jina”alisema Lilian.


Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa ya Tanzania bara na Visiwani Zanzibar wanapatiwa mafunzo ya siku nne ya usalama mtandaoni na kupambana na ukatili wa kijinsia mtandaoni yanayolenga kuwajengea uwezo wa kujilinda kwa kutumia njia mbadala mkoani Morogoro.


Afisa Programu wa Mafunzo na Machapisho kutoka UTPC Victor Maleko alisema mafunzo hayo yamelenga kutoa mbinu za kujilinda kwa waandishi wa habari wanawake juu ya usalama mtandaoni na kupambana na ukatili wa kijinsia mtandaoni.


Victor alisema usalama wa ulinzi unaanza na mwandishi mwenyewe binafsi kwa kujilinda hasa katika kuelekea katika kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na mawadini katika maandamano, mikutano ya kisiasa, kuepuka kuvaa nguo ambazo hazilengi chama chochote lakini kukaa eneo ambalo endapo itajitokeza vurugu iwe rahisi kuondoa eneo hilo kwa urahisi.


“Mafunzo haya yameandaliwa na UTPC ikishirikiana na Internation Media Support, Jamii Africa, Nukta Afrika na Tamwa na tunawaomba wenzetu wa vyombo vya usalama, vyama vya siasa viendelee kuwa na wajibu wa kumlinda mwandishi katika majukumu yao na kumekuwa na madhira ambayo wanayapata waandishi wa habari wanawake na wanaume na mwaka 2024 madhi 20 tulirekodi ikihusisha waandishi 28.”alisema Victor.


Victor aliongeza kuwa UTPC mwaka 2021/2022 ilirekodi jumla ya madhira 23 na mwaka 2023 madhira 18 yalipungua kwa sababu walitoa mbinu mbalimbali kwa waandishi wa habari za kujilinda na kuepuka vitendo vya ukatili wakati Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) mwaka 2023 ikirekodi madhira asilimia 77.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI