Header Ads Widget

TANAPA KUFANYA MABORESHO KITUO CHA MALIKALE UJIJI

 

Kituo cha Malikale cha kumbukumbu ya Dk.David Livingstone kilichopo Ujiji mjini Kigoma
Miriam Mkonya Mhifadhi Mkuu wa kituo cha Malikale cha Kumbukumbu ya Dk.David Livingstone Ujiji mjini Kigoma akitoa maelezo kuhusu historia mbalimbali za enzi ya utumwa zilizopo kituoni hapo

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kufanya maboresho makubwa katika kituo cha Malikale cha Kumbukumbu ya Dk.David Livingstone kilichopo Ujiji mjini Kigoma ili kuvutia idadi kubwa ya wageni wa ndani na nje ya nchi kutembelea vivutio hivyo.


Mhifadhi Mkuu wa kituo cha Malikale cha Ujiji Kigoma,Miriam Mkonya akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo alisema kuwa tayari wameshaandika maombi ya kwa ajili ya mpango huo na TANAPA imeshapitisha hivyo wanasubiri kuanza kwa utekelezaji wa mpango huo.


Mkonya alisema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo wanatarajia kuweka ni kuongeza vivutio vya kiasili, kuweka maeneo ya burudani kwa wageni ikiwemo vyakula vya kiasili lakini pia kuweka mabembea kwa watoto na michezo mbalimbali.


Aidha alisema kuwa pamoja na kituo hicho pia mpango huo unalenga kuitangaza njia ya kati iliyokuwa ikitumiwa na watumwa kutoka Ujiji Kigoma kupitia Kwihara mkoani Tabora, kilimatinde Singida, Kongwa Dodoma hai kufika Bagamoyo mkoani Pwani ambapo watumwa na wapagazi waliokuwa wakibeba pembe za ndovu walitumia.


Kwa upande wake Mhifadhi wa malikale wa kituo hicho, Kassim Govora alisema kuwa njia ya kati ya utumwa kutoka Ujiji hadi Bagamoyo ina historia kubwa kwenye masuala ya mambo ya kale nchini hasa kumbukumbu ya biashara ya utumwa hivyo watu wengi wanapaswa kutembelea kivutio hicho kuona uhalisia wake.


Govora ambaye ametembea njia hiyo yenye urefu wa kilomita 1200 anaeleza kuwa njia hiyo ina historia kubwa ndani na nje ya nchi lakini wageni ambao hawajafika hapo wanaweza kuona ni kitu kidogo akieleza kuwepo kwa historia pia ya kanisa katoliki lenye miaka 140 likiwa kanisa la kwanza mkoani Kigoma.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI