Header Ads Widget

RAIS DK. SAMIA AZINDUA VIWANDA VIWILI VYA MOLI OIL MILLS Co. LTD.


 


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amezindua viwanda viwili ambavyo ni Kiwanda cha kuchakata Mabomba pamoja na kiwanda cha kuchakata pamba.


Dk. Samia amezindua viwanda hivyo katika eneo Salunda, lilioko Halmashauri ya Mji Bariadi Mkoani Simiyu ambapo ameridhishwa na uchakataji wa zao la Pamba katika Kiwanda hicho.


Viwanda hivyo vyenye thamani ya shilingi Bil. 8 vinamilikiwa na kampuni ya Moli Oil mills company LTD ambao pia ni wamiliki Makampuni ya Nsagali.


Akizungumza na Wananchi mara baada ya uzinduzi huo, Rais Dk. Samia ameupongeza uongozi wa Kampuni hiyo kwa uwekezaji mkubwa walioufanya ambao umelenga kutoa ajira.


"Ndugu yetu huyu ametufanya tusitumie fedha za kigeni kununua mabomba nje ya Nchi, na badala yake tutanunua bidhaa za ndani, hivyo nawapongeza kwa kufungua kiwanda cha Pamba na mabomba" amesema.


Ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kuzingatia ubora na viwango wakati wa uzalishaji wa bidhaa za Pamba na mabomba.


Viwanda hivyo vimezalisha takribani ajira 850 za moja kwa moja pamoja na ajira nyingine 400 kwa wanufaika wa nje huku kikitoa fursa kwa wajasiliamali wadogo wadogo kunufaika kwa kufanya biashara za mama lishe.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa June 19, 2025



Mwisho.














Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI