NA MATUKIO DAIMA MEDIA
Kampuni ya JND Polybags ya mkoani Iringa imeendelea kuimarisha uzalishaji wa vifungashio vya kisasa vinavyotumika kwenye sekta mbalimbali, hatua inayolenga kuimarisha utunzaji Mazingira na ukuzaji ajira kwa vijana.
Akizungumza na Matukio Daima Media Meneja Masoko wa kampuni hiyo Jeremia Richard Kasililika amesema kuwa JND Polybags imewekeza katika teknolojia ya kisasa inayowezesha kuzalisha viroba vyenye ubora wa kimataifa kwa matumizi ya kilimo, biashara, na viwanda vikubwa.
“Kampuni yetu inajihusisha na utengenezaji wa vifungashio hususani vya kuhifadhia nafaka na kampuni hii iliazishwa tangu mwaka 2023 ikiwa imebase na utengenezaji wa vifungashio vya nafaka katika mikoa ya nyanda za juu kusini ikiwemo Iringa,Mbeya na Njombe na mikoa hii ni mikoa ambayo inajihusisha na kilimo lakini kwa bahati mbaya hapakuwa na kiwanda cha kuzalisha vifungashio na kupitia hilo kampuni hii iliamua kuja na kiwanda cha kutengeneza vifungashio ili kurahisisha huduma kwa wakulima.
Aidha Kasililika ameelezea umuhimu wa kuanzishwa vifungashio vipya vya “JND shopping bag” huku akiongeza kuwa kampuni hiyo inalenga kutoa suluhu ya vifungashio imara vinavyodumu kwa muda mrefu na kuzingatia sera ya taifa ya usimamizi wa taka za plastiki ili kulinda mazingira.
“Kwa vision kubwa ambayo kampuni yetu inayo, haikuishia hapo tu katika kuzalisha vifungashio vya kuhifadhia nafaka iliweza kuangalia kwa jicho jingine na ikaja na vifungashio vipya kabisa kwa mwaka huu vya “JND shopping bag” vyenye uwezo wa kubeba kilo 5 mpaka 10 ni vifungashio imara na vinaweza kutumika zaidi ya mara moja.
0 Comments