Hossein Salami, kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC), aliyeuawa katika mashambulizi ya Israeli mapema Ijumaa, ni kiongozi mwandamizi zaidi wa Iran kufa katika mashambulizi hayo.
Salami, ambaye alikuwa na umri wa miaka 65, alijulikana kwa kuchukua msimamo mkali dhidi ya wapinzani wa Iran, ikiwa ni pamoja na Israel na Marekani. Mwezi uliopita tu, alikuwa ameonya kwamba Tehran "itafungua milango ya kuzimu" ikiwa itashambuliwa na nchi yoyote.
Israel ilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Iran, ikisema ililenga vituo vya nyuklia, viwanda vya makombora ya balistiki na makamanda wa kijeshi, licha ya Rais wa Marekani Donald Trump kumuonya mshirika wake dhidi ya kuvuruga mazungumzo juu ya makubaliano ya nyuklia.
Tehran imeonya kuwa Israeli na Marekani ambazo zinakanusha kuhusika zitalipa "gharama kubwa" kwa mashambulizi hayo, na kuibua wasiwasi kwamba hii itasababisha eneo ambalo tayari ni dhaifu kuztumbikia katia hali ya vita kamili.
Mashambulizi ya Israeli pia yalimuua Mohammad Bagheri, Mkuu wa jeshi la la nchi hiyo, Gholamali Rashid, naibu kamanda wa jeshi la Iran, na wanasayansi kadhaa wa nyuklia
Siku moja tu kabla ya mashambulizi hayo, Salami alikuwa amesema kwamba Iran ilikuwa "tayari kabisa kwa hali yoyote, kwa hali na hali".
"Adui anadhani anaweza kupigana na Iran jinsi inavyopigana na Wapalestina wasio na ulinzi ambao wako wamezingirwa na Israeli," alisema. "Tumejiandaa kwavita na tuna uzoefu."
Salami alijiunga kwa mara ya kwanza na Walinzi wa Mapinduzi - tawi lenye nguvu la vikosi vya jeshi la Iran - mnamo 1980 wakati wa vita vya Iran na Iraq na kuwa naibu kamanda mnamo 2009, kisha kamanda kwa muongo mmoja baadaye.
Tangu miaka ya 2000, amewekewa vikwazo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Marekani kwa kuhusika kwake katika mipango ya nyuklia na ya kijeshi ya Iran.
Salami alijivunia uwezo wa kijeshi wa Iran, wakati mmoja akitangaza kwamba nchi hiyo ilikuwa "kwenye hatihati ya kuwa taifa lenye nguvu ulimwenguni".
Kufuatia shambulio la Israeli dhidi ya malengo ya Iran nchini Syria mnamo 2019, Salami aliapa "kufuta utawala wa Kizayuni" kwenye ramani ya kisiasa.
Kufuatia shambulio lingine mwezi Aprili mwaka jana dhidi ya ubalozi wa Iran nchini Syria, ambalo liliwaua wanachama saba wa Walinzi wa Mapinduzi wakiwemo majenerali wawili, Salami alitoa onyo kama hilo: "Watu wetu jasiri watauadhibu utawala wa Kizayuni."
Iran na Israeli walikuwa washirika hadi mapinduzi ya 1979 nchini Iran, ambayo yalileta utawala ambao umetumia kupinga Israeli kama sehemu muhimu ya itikadi yake.
Utawala wa Irani leo hautambui haki ya uwepo wa taifa la Israeli. Kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei, ameiita Israeli "uvimbe wa saratani" ambao "bila shaka utang'olewa na kuharibiwa".
Israel inasema matamshi ya Tehran yanaifanya Iran kuwa tisho lililopo. Israel na washirika wake pia wamekosoa kuongezeka kwa vikosi vya wakala vya Iran katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kundi la wanamgambo wa Shia la Lebanon la Hezbollah ambalo limeapa kuiangamizwa Israeli.
Salami na maafisa wengine waandamizi wa Walinzi wa Mapinduzi mara kwa mara humshauri kiongozi mkuu wa Iran.
Walinzi wa Mapinduzi wa Iran ni akina nani
Kiongozi Mkuu wa kidini wa Iran alianzisha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 40 iliyopita ili kutetea mfumo wa Kiislamu wa nchi hiyo na kutoa vikosi vya kawaida vya jeshi, ambavyo hawakuviamini.
Likiwa na zaidi ya wafanyikazi 190,000 wanaofanya kazi na kujivunia vikosi vyake vya ardhi, jeshi la wanamaji na angani, Walinzi wa Mapinduzi ni moja wapo ya vikundi vyenye nguvu zaidi na vinavyoogopwa zaidi vya kijeshi na kisiasa.
Wakati jeshi la Iran linalinda eneo la nchi hiyo, Walinzi wa Mapinduzi walianzishwa kwa ajiliya kuilinda serikali yenyewe.
Wakati kikundi kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu, nguvu zake haziangaliwi kwa urahisi na taasisi zingine.
Kikundi hicho kinasimamia silaha za kimkakati za Iran na kinadhibiti Kikosi cha Upinzani cha Basij, ambacho mara nyingi kimekuwa kikitumiwa kukandamiza upinzani wa ndani.
Walinzi wa Mapinduzi pia wanadhaniwa kudhibiti karibu theluthi moja ya uchumi wa Iran kupitia safu ya kampuni tanzu na amana. Pia kinashikilia mabilioni ya dola katika mikataba ya ujenzi na uhandisi.
Kwingineko katika Mashariki ya Kati, kikundi hicho kina ushawishi kwa kutoa pesa, silaha, teknolojia, mafunzo na ushauri kwa serikali washirika.
Baadhi ya wanachama wasomi zaidi wa Walinzi wa Mapinduzi wanaendesha kitengo chake cha kivuli cha operesheni nje ya nchi, Kikosi cha Wakurdi, ambacho kina uhusiano na vikundi vyenye silaha katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Afghanistan, Iraq, Lebanon, maeneo ya Palestina, na Yemen.
Maafisa wa zamani wa Walinzi wa Mapinduzi wanaendelea kushika nyadhifa zenye ushawishi katika serikali, bunge na vyombo vingine vya kisiasa. Ni pamoja na Rais wa zamani Mahmoud Ahmadinejad na spika wa zamani wa bunge Ali Larijani.
0 Comments