NA MATUKIO DAIMA MEDIA TUPIGIE 0754026299
WAKATI leo zoezi la uchukuaji fomu za kuwania nafani mbali mbali ikiwemo ya ubunge na udiwani kwa watiania wa chama cha mapinduzi (CCM) limeanza rasmi ,aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini kwa vipindi viwili tofauti kupitia CHADEMA mchungaji Peter Msigwa amejitokeza kuchukua fomu.
Mchungaji Msigwa amekuwa mwana CCM wa kwanza kufika kuchukua fomu majira ya saa 2:00 asubuhi .
Matukio Daima Media ilikuwepo viwanja vya CCM wilaya ya Iringa mjini toka saa 1:35 asubuhi huku Msigwa akifika saa 1:39 asubuhi akiwa na dereva wake na Leonce Marto ambae pia alijiunga CCM akiyokea chadema .
Akimkabidhi fomu hiyo ya ubunge baada ya kuilipia kiasi cha Tsh 500,000 katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Hassan Makoba alisema wajibu wa kila mtia nia kwenda kujaza fomu na kurejesha pia anatakiwa kuheshimu kanuni za CCM na kuepuka kuanza kampeni kabla ya muda pamoja na kungatia makatazo mengine yote.
Makoba alisema zoezi hilo limeanza na kuwa mwanachama wa kwanza kupewa fomu hiyo ni Peter Msigwa ambae amefika mapema zaidi japo alitoa wito kwa wanacha wengine kuendelea kujitokeza.
Akijibu maswali ya waandishi baada ya kuchukua fomu Mchungaji Msigwa alisema kuwa iwapo atashinda kura za maoni na waanchi wa Iringa mjini wakimchagua kuwa mbunge atakuwa mbunge wa kuwasemea wananchi bungeni kama ilivyokuwa wakati akiwa mbunge.
kuhusu kauli mbio ya No Reform No Election na ile ya Kazi na utu Tunasonga mbele alisema kuwa hizo ni kauli mbiu japo anaamini katika Oktoba tuna tiki na kazi na Utu tunasonga mbele kwani matunda yanaonekana na serikali ya CCM chini ya Rais Dkt Samia imefanya mengi hivyo watanzania kuachana na kauli mbiu zisizo na tija za No Reform No Election.
TAZAMA MAHOJIANO YOTE MATUKIO DAIMA TV ⬇️⬇️⬇️
TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
0 Comments