Na Lilian Kasenene,Morogoro
Matukio DaimaApp
JESHI la Magereza nchini limesema kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imekuwa na msaada kwa wafungwa na maabusu 12,000 ambapo kati yao maabusu 6,900 wametoka baada ya kupata usaidizi wa kisheria.
Hayo yalielezwa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza CP Nicodemus Tenga wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa sheria, urekebu wa jeshi la magereza kuhusu huduma za msaada wa kisheri, mapokezi ya wafungwa magerezani na adhabu mbadala
Kamishna Tanga alisema kwa minajiri hiyo idadi ya wafungwa kwenye magereza kwa mwaka 2021 ni zaidi ya 32, 000 lakini kwa mwaka 2025 hadi june 09, idadi ya wafungwa imepungua hadi kufikia 26,896
“Kwa uwiano tuliokuwa nao kipindi hicho tulikuwa na wafungwa na maabusu nusu kwa nusu lakini tunavyoongea sasahivi wafungwa asilimia 75, na maabusu asilimia 25. Na kwa taarifa Uwezo wa magereza yetu ni wafungwa 29,102 lakin kwa leo i tunaupungufu wa zaidi ya wafungwa 3000 kwa maana yake kuna nafasi” alisema Tenga
Alisema jeshi hilo la magereza lina jumla ya vituo 129, vituo vya mikoa 26 na vituo vingine vya vikosi pamoja na shule vipo 6 ambapo jumla yake 32 hukui Wilaya 50 zikiwa hazina magereza hivyo wafungwa wake wanalazimika kupelekwa kwenye magereza ya wilaya jirani akitolea mfano Wilaya ya Kakonko na Uvinza.
Nae mkurugenzi wa Katiba na ufuatiliaji haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Jane Lyimo alisema uwepo wa mafunzo hayo yanalenga moa kwa moja kuongezea uelewa kuhusu haki za binaadamu, usimamizi haki za wafungwa, utekelazaji wa adhabu mpadala, usimamizi wa mikataba
“Tunatarajia kutoka kwenu kuzingatia haki za binadamu, kujenga mfumo wa haki unatenda kazi kwa ufanisi, uwazi na kwa kutumia ushahidi wa kisheria” alisema Lyimo
Mkurugenzi huyo alisema mafunzo hayo yaliyofanyika kwa awamu mbili yameshirikisha washiriki 290 kutoka mikoa yote nchini ikiwa ni kuonyesha dhamira ya serikali katika kuimarisha mnyororo wa haki jinai.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakam Maswi, Naibu Katibu Wizara hiyo Franklin Rwezimula alisema Jeshi la Magereza limebeba dhamana kubwa isiyopaswa kubezwa, dhamana ya kusimamia hatua ya mwisho kabisa ya mnyororo wa haki jinai.
Alisema jukumu hilo linahitaji ujuzi wa kitaalamu, uelewa mpana wa sheria mbinu za urekebu wa tabia, uadilifu hali ya juu na uwezo kufanya kazi katika mazingira yenye changamoto mbalimbali.
“Katika Dunia ya sasa inayokumbwa na mabadiliko ya kasi katika nyanja mbalimbali hususani kiusalama, kijamii na kisheria ni wajibu wenu jeshi la magereza, kama Taifa kuwekeza kwa makusudi katika uimarishaji wa uwezo wa watumishi wa umma”
Mwisho.
0 Comments