Na Shomari Binda-Musoma
MADIWANI wa viti maalum manispaa ya Musoma wamesoma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020,2025 na kuelezea mafanikio waliyoyapata.
Utelezaji huo wameusoma leo juni 19,2025 kwenye baraza maalum la UWT lililofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara.
Madiwani waliosoma utekelezaji wa ilani hiyo ni Naima Minga,Amina Masisa,Arieth Kumila,Asha Muhamed na Meryciana Masasi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa usomaji taarifa wamesema wanajivunia ushirikiano walìupata kutoka kwa viongozi na wanachama wa UWT.
Wamesema moja ya mafanikio ni kuhakikisha wanaanzisha vikundi vya wanawake na kuvisajili na baadae kupata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.
Licha ya eneo hilo madiwani hao wamezungumzia pia namna walivyoshiriki shughuli nyingine za kijamii pamoja na utekelezaji wa miradi.
Aidha madiwani hao wamewaomba muda ukifika wajumbe waendelee kuwaamini na kuwachagua tena muda ukifika kutokana na namna walivyofanya kazi.
0 Comments