Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa Kenani Kihongosi ameongoza maelfu ya waombolezaji kumzika Edo Bashiri aloyekuwa mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa mjini na mtangazaji wa radio Ebony Fm.
Mbali ya kenani viongozi wengine walioshiriki nae ni MCC Salim Abri Asas,MNEC Richard Kasesela na Livingistone Lusinde,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin na wenyeviti wote wa CCM wilaya za mkoa wa Iringa na jarani
pia wafanyabiashara mbali mbali akiwemo mkurugenzi wa Maji CF Chesco Ng'umbi,Arif Abri mkurugenzi wa FM Abri ambae pia mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa ,Dickson Mwipopo mkurugenzi wa shule za Real Hope ambae pia mjumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Iringa,Evarsto Mfugale mkurugenzi wa Radio Ebony Fm ,Jimson Kisigo mkurugenzi wa JND na wengine wengi.
Huku wabunge wa mkoa wa Iringa walioshiriki msiba huo ni pamoja na mbunge wa vijana Taifa Jasmin Ng'umbi,mbunge wa Isimani Emanuela Mtatifikolo ,mbunge wa Kilolo Ritta Kabati,mbunge wa Mafinga Dickson Villa ,mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Nacy Nyalusi,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Fadhili Ngajilo.
Hata hivyo msiba huo ulihudhuriwa na wananchi wa kada mbali mbali kutoka maeneo mbali mbali na kupelekea kujaza uwanja wa mpira wa KKKT Kibwabwa .
Akizungumza katika mazishi hayo MCC Asas alishauri wananchi kujenga utamaduni wa kusaidiana wakati wa ugonjwa na kuwa kwa upande wake na viongozi wa CCM walikuwa jirani sana na Edo toka akiwa Hospital ya Wilaya Frelimo na baadae kumpeleka Rufaa mkoa wa Iringa.
Hata hivyo alisema kifo cha Edo ni pigo kubwa na kwa upande wake ataendelea kuisaidia familia hiyo na kutaka wananchi kuendelea kumjulia hali bibi wa Edo ambae ni mzee.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin alisema wakati wa misiba ni wakati wa kuomboleza na kumzika marehemu na sio wakati wa kuibua migogoro na kuwa CCM imeshiriki msiba huo wa asilimia zote na hata eneo la uwanja wa kuagia mwili ni familia ndio ilipendekeza hapo ni si kweli kama CCM imezuia uwanja wa Samora.
pia Yassi alisema CCM mkoa wa Iringa inaikabidhi familia hiyo Tsh milioni 10 kwa ajili ya kuiunga mkono .
Mbunge wa Iringa mjini Fadhili Ngajilo aliomba Edo aendelee kuenziwa na ikiwezekana mtaa mmoja upewe jina lake.
Mwenzezi CCM Taifa Kenani Kihongosi alisema kwa kutambua mchango wa Edo katika tasini ya habari na Chama suala la kutenga mtaa mmoja kupewa jina lake halikwepeki na kuiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kufanya wepesi kushughulikia hilo huku akichangia Tsh milioni 10 kuipa familia yake.


































0 Comments