Header Ads Widget

GRACE TENDEGA AVUTIWA NA KAZI ZA RAIS SAMIA ACHUKUA FOMU UBUNGE KALENGA AWASHAMBULIA VIKALI CHADEMA ASEMA NO REFORM KALENGA WAJAIELEWA ZAIDI YA OKTOBA TUNATIKI..

 


NA MATUKIO DAIMA APP.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa   Grace Tendega amejitokeza kuchukua fomu  ya kugombea Ubunge jimbo la Kalenga kupitia chama cha Mapinduzi(CCM) huku akiijaza na kurehesha muda mfupi.

Tendega alifika asubuhi ya Juni 28  katika ofisi za wilaya ya Iringa vijijini kuchukua fomu hiyo  na kuirejesha majira ya saa 9:30 Alasiri huku akieleza kuwa watanzania wameona kazi ambazo zimefanywa na chama cha mapinduzi kwa ilani yake ya miaka mitano.

Alisema watanzania wameona kazi na jitihada kubwa za Rais Samia ambazo amezifanya kwa kuweza kuhakikisha kwamba nchi inakuwa na utulivu amani na taratibu mbalimbali za kimaendeleo.

"Mh Rais ameweza kuleta falsafa ya 4R ambayo inahakikisha watanzania wanaelewa kuwa wanahitaji mambo makubwa ambayo ameyaeleza kuwa tunahitaji kuwa na maelewano ambayo yamefanyika, amefanya maridhiano na taasisi pamoja na vyama mbalimbali "


akizungumzia falsafa ya 'No Reform, No Election' Tengega alisema kuwa watanzania wengi hawajaelezwa nini maana ya falsafa na inafanya kazi namna gani.

"Endapo watanzania wangeelewa namna inavyofanya kazi wangeelewa lakini tunaona kutokana na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu no reform no election wanaona kama inawanyima kuwa na fursa za kugombea na kupiga kura kwa watanzania wengine"

Aliongeza kuwa kugombea na kupiga kura ni fursa ya kikatiba kwa mtu yeyote anayehitaji kugombea nafasi yeyote uongozi kwa kufuata katiba.


Akizungumzia kwa upande wa falsafa ya Oktoba tunatiki alisema kuwa CCM imefanya mambo mengi makubwa na mazuri kuanzia elimu,afya 

"Shule za watoto wa kike zimejengwa kwa wingi na kuondokana na ukatili kwa watoto wa kike waliokuwa wanafanyiwa,kuna zahanati na vituo vya afya 


Rais amepata pesa za mikopo kwa ajili ya kuja kufanya kazi hizo ambazo zimerejea kwa wananchi ambapo wangesema serikali ifanye kwa kodi za wananchi wangedunduliza na wasingeweza kuoa miradi mingi ikitekelezwa kwa haraka na ufanisi.

"Fedha ya mkopo imefanya kazi na inaonekana,hivyo watanzania waache kubeza kuhusu deni la taifa badala yake waunge mkono na kumchagua tena ili aweze kukamilisha yale aliyoyaanza"alisema

alisema endapo atapata fursa ya kuteuliwa kugombea Ubunge jimbo la Kalenga ataeleza nia yake na lengo kuu ni kuwasemea wananchi wa kalenga ili waweze kupata maendeleo na fursa mbalimbali.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI