Header Ads Widget

DEREVA WA GARI YA CHADEMA AKAMATWA NA POLISI KWA KUSABABISHA AJALI


NA MATUKIO DAIMA MEDIA MOROGORO

Polisi wachunguza kifo cha fundi mkongwe  ambaye mabaki ya mwili wake yamekutwa Makaburi ya Kolla

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Yahaya Bakari Idd (43), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, kwa tuhuma za kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali iliyohusisha gari la Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo SACP  Alex Mkama, ajali hiyo ilitokea Juni 5, 2025, katika eneo la Mataa ya Tumbaku, Kata ya Mafisa, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda Mkama alieleza kuwa gari aina ya Ford Ranger lenye namba za usajili T.661 DQL, mali ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), liliacha njia na kugonga lori la Scania lenye namba T.340 DWW lenye tela namba  T.976 CJE lililokuwa limeegeshwa katika kisima cha mafuta.

Katika ajali hiyo, abiria watatu waliokuwa ndani ya Ford Ranger walijeruhiwa kwa kiwango kidogo, wakapatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Aidha Polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu kifo cha fundi ujenzi, Odilo Anania Sumi (80), ambaye hakuwa na makazi maalum. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, mabaki ya mwili huo yalikutwa katika eneo la makaburi ya Kola, Manispaa ya Morogoro, siku hiyo hiyo ya Juni 5, 2025.


Kamanda Mkama alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa akiishi maisha ya mtaani, na mwilini mwake kulikutwa sehemu ya nguo, baadhi ya dawa, na karatasi yenye namba za simu.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI