Na Shomari Binda-Musoma
WAZIRI wa Madini Antony Mavunde ameupongeza mkoa wa Mara kwa kasi ya ukuaji kwa sekta ya madini na kuufanya mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa bora.
Kauli hiyo ameitoa leo juni 6,2025 kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo wakati akihitimisha maonyesho ya kwanza ya madini mkoani Mara
Amesema mkoa wa Mara unakuja juu katika sekta ya madini kwa kusaidia pato la mkoa na taifa kwa ujumla na juhudi hizo zinafanywa na mlezi wa wachimbaji mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi na wadau wengine.
Amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inakuja na neema kubwa kwa wachimbaji kwa kuhakikisha kupitia sekta hiyo wanainuka kiuchumi.
Waziri Mavunde amesema ili kuona mambo mazuri yanaendelea kufanikiwa katika mambo 16 ya kuboresha sekta ya madini ni pamoja na kuanzisha vituo vya ukodishaji mitambo na wachimbaji wadogo kuchimbiwa kwenye maeneo yao.
Amesema serikali serikali inaendelea kuwasaidia wachimbaji wadogo ili kuachana na uchimbaji wa kubahatisha na kutumia nguvu za giza na kuja na dira ya kupima chini ya ardhi na kubaini maeneo yenye madini.
" Nianze kwa kutoa pongezi zangu kwa uongozi wa mkoa wa Mara chini ya mkuu wa mkoa Kanali Evans Mtambi kwa juhudi kubwa za kuinua na kuja kwa kasi kwenye sekta ya madini.
" Maonyesho haya yameandaliwa kea ufanisi mkubwa na imani yangu baada ya hapa tutapaa juu kwenye sekta hii ya madini hapa nchini",amesema.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo nchini John Bina amesema serikali chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan inawatendea haki wachimbaji na hawapaswi kulalamika bali kuongeza juhudi kwenye shughuli zao.
Awali mkuu wa mkoa wa Mara kama mlezi wa wachimbaji wadogo mkoa wa Mara amesema wataendelea kuwasimamia vizuri wachimbaji wadogo na kuhakikisha wanakua
Amesema sekta ya madini inachangia pato la mkoa kwa asilimia 18 na kwa namna mambo yanavyokwenda vizuri wataendelea kuchangia zaidi.
Mapema asubuhi wachimbaji wadogo na wadau wa madini walifanya matembezi ysliyoanzia ofisi ya mkuu wa mkoa hadi viwanja vya shule ya msingi Mukendo kumpongeza na kumshukuru Rsis Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyosaidia kukuza sekta madini nchini.
Maonyesho hayo ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani Mara yameonekana kuwa na mafanikio makubwa.
0 Comments