Header Ads Widget

DARAJA LA MAKELENG'ENDE KUKAMILIKA SEPTEMBER 2025

 

NA HADIJA OMARY 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail ally usi amekagua na kuridhishwa na uendelevu wa ujenzi wa Daraja la Makeleng'ende linalojengwa Katika Barabara kuu kutoka Dar es salaam kwenda Mikoa ya Kusini Eneo la njia nne linalojengwa na mkandarasi Makapu contraction 

Akizungumza mara baada ya kuona uendelevu wa Daraja Hilo bwana Usi aliwaomba wananchi kuendelea kuwa wavumili wakati Serikali ikiendelea na ujenzi huo na pasinashaka Daraja Hilo litakamilika kwa wakati na wananchi wataanza kulitumia 

Meneja wa wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS ) Mkoa wa Lindi Mhandisi Emily Zengo akitoa taarifa kwa kiongozi huyo amesema Daraja hilo ni ambalo  miongoni mwa madaraja yaliyoathiriwa na mvua za El-nino na Kimbunga Hidaya ambao  unatekelezwa na Mkandarasi Mzawa M/S Makapo Contractors and General Supplies Company Ltd kwa gharama ya Shilingi 11,116,536,032 .

Amesema Mradi huo unahusisha ujenzi wa boksi Kalvati maeneo ya Mtandago na Masaninga na ujenzi wa barabara ya kuingia darajani yenye urefu wa km 2.

Aidha Mhandisi Zengo alisema kuwa Serikali imetoa fedha nyingi Mkoani Lindi kurejesha miundombinu iliyoathiriwa na Mvua za El-nino na Kimbunga Hidaya ambapo Jumla ya Shilingi 119,130,009,067 zimeletwa kwaajili ya ujenzi wa madaraja mbalimbali katika barabara za Marendego-Mingoyo,Tingi-Kipatimu,Nangurukuru -Liwale.

Nyingine ni Liwale -Nachingwea na Kiranjeranje -Namichiga -Ruangwa ambapo kukamilika kwa ujenzi wa madaraja hayo kutatachua changamoto za usafiri hasa wakati wa mvua.

Wananchi wa Kijiji cha Njia nne Wilayani Kilwa Mkoani Lindi wamesema wanafurahia hatua ya serikali kupitia Wakala ya Barabara nchini Tanroads kuendelea na ujenzi wa daraja la Mikereng’ende lenye urefu wa mita 40 uliofikia asilimia 51.5.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI