Na Fadhili Abdallah,Kigoma.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kuchafuana, mbwembwe na mambo ambayo yamekatazwa katika kanuni na taratibu za chama hicho kufanywa na wagombea au wapambe wao katika kuchukua fomu katika hatua hii ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge na udiwani katika uchaguzi Mkuu itakuwa moja ya vigezo vitakavyowaengua wagombea kwenye uchaguzi huo.
Katibu wa uenezi,siasa na mafunzo CCM mkoa Kigoma, Deogratius Nsokolo amesema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchaguzi huo na kubainisha kuwa kitendo cha mgombea mmoja kumchafua mwingine kwa namna yeyote itakuwa moja ya vigezo ambavyo vitafanya mgombea kuenguliwa.
Nsokolo alisema kuwa CCM imeshatoa maelekezo kwa wanachama wote wa CCM wenye nia ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge na udiwani kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu hivyo kanuni na taratibu zilizowekwa na chama zinapaswa kusimamia kikamilifu na wanachama wote ikiwemo kuzuia maandamno, matarumbeta au misafara mikubwa ya magari na pikipiki kusindikiza wagombea.
Kwa sasa mkoa Kigoma una kata 139 na majimbo manane ya uchaguzi ambayo yataingia kwenye mchakato wa uchaguzi ambapo Ktibu Mwenezi huyo wa CCM mkoa Kigoma amewatahadharisha viongozi na wanachama kuwa watulivu na kufuata miongozi iliyowekwa ili kutowaharibia watia nia wao.
Katika hatua nyingine Nsokolo ametangaza kuwa hatagombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Nsimbo mkoa wa Katavi kama alivyoonesha nia awali na kwamba kwa sasa anabaki kama mtumisho mtiifu ndani ya chama na kwamba nia yake ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo iko pala pale lakini siyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwisho.
0 Comments